MATANGAZO

/zest+mkali+3.jpg /TULAMCHA+2+copy.jpg

Thursday, 1 August 2013

UJIO WA BALE RAIS WA ZAMANI WA REAL MADRID APEWA ASILIMIA

RAIS wa zamani wa Real Madrid, Ramon Calderon anaamini kuwa klabu hiyo inapigana kusaka saini ya Gareth Bale kwa ajili ya kuchukua nafasi ya Cristiano Ronaldo aliye ‘mguu ndani mguu nje.
Madrid imewasilisha ofa rekodi ya dunia ya pauni milioni 85 kwa ajili ya kumnasa winga huyo wa Wales ambaye ameweka wazi nia yake ya kutaka kuondoka White Hart Lane.
Lakini Calderon amedai kuwa mrithi wake wa kiti cha urais, Florentino Perez anakazania kumpata Bale ili kuziba pengo litakaloachwa na Ronaldo kama ataondoka.
Staa huyo Mreno amekuwa akihusishwa kwa muda mrefu na mpango wa kurudi katika klabu yake ya zamani ya Manchester United, na ameripotiwa kutaka mshahara mkubwa ambao Real ‘itakuwa ngumu kukubali kumpa’ ili asaini mkataba mpya.

Calderon anasema kutua kwa Bale kunakosubiriwa kwa hamu kubwa ili kutuliza mashabiki Bernabeu ni wazi kutamsukuma Ronaldo mwenye umri wa miaka 27 kuchagua kutosaini mkataba mpya wa kuendelea kubaki.
“Najua kwamba yeye (Ronaldo) hana furaha kutokana na tabia na mwenendo wa rais (Perez). Ameomba euro milioni 20 kila msimu jambo ambalo litakuwa gumu kwa Real kukubali,” Calderon aliiambia shoo ya Drive Time ya talkSPORT.
Calderon amesema kuwa hisia zake zinamwambia kuwa Perez ana hofu kuwa Ronaldo atasema hataki kuendelea, ambayo itakuwa habari mbaya kwa Madrid.
“Angependa kumuona akistaafia Real, lakini sasa hali ni ngumu. Acha tuone katika kipindi cha wiki zijazo au miezi kama kutapatikana utatuzi na anaweza kubaki,” alisema Calderon.
Bale alimwambia bosi wake Andre Villas Boas kwamba anataka kujiunga na Carlo Ancelotti Real Madrid katika siku yake ya kwanza ya kurudi mazoezini baada ya ofa ya kusisimua kutoka Bernabeu.
CHANZO CHA HABARI HII NI SALUTI 5 ,SAID MDOE

No comments:

Post a Comment