MKALI wa muziki wa bongo fleva nchini, Naseeb Abdul ‘Diamond Platinum’, amefunguka mengi juu ya historia ya maisha yake na changamoto alizozipitia katika safari yake ya muziki mpaka kufikia hapa, katika semina ya Fursa, iliyoandaliwa na Clouds Fm katika kila mkoa tamasha la Fiesta linapopita. Diamond
alikuwa
ni mmoja wa wasemaji, watoa maada mbele ya mamia ya wakazi wa Tabora
katika kuhamasisha vijana kuzijua fursa na kuzitumia ili kujiletea
maendeleo katika maisha yao. Kwa mujibu wa Diamond, mwaka 2008 na 2009
alikuwa akifanya kazi katika kiwanda cha mabegi kilichoko Mikocheni na
kulipwa mashahara wa shilingi 2,000 kwa masaa 8, huku nauli ikimgharimu
shilingi 1,000 mpaka kufika kwao na hapo chakula ni zaidi ya shilingi
1,000. “Ukimuona mtu ana mafanikio kiukweli ujue amehangaika sana, mimi
katika maisha yangu sikuwahi kufikiria kama ningelikuja kupanda ndege
kwa kutumia pesa yangu, namshukuru sana Mungu na haya ni matunda ya kazi
ngumu ambazo huwa nazifanya,” alisema. Msanii huyo aliwataka wapenzi wa
kazi zake kufanya kazi kwa bidii kwa kipindi kifupi ili kufanikiwa
katika maisha yao na kuonekana watu katika jamii na sio kudharaulika.
No comments:
Post a Comment