Muimbaji wa ‘Niwe Nawe Milele’ Rehema Chalamila aka Ray C jana alifanya interview ya kwanza ya TV tangu takriban miezi 10 iliyopita baada ya kujichimbia kupata matibabu ya madhara aliyokuwa amepata kutokana na matumizi ya madawa ya kulevya.
Akiwa na muonekano mpya, mchangamfu, aliyenawili, mrembo na mwenye afya njema, Ray C alizungumza kwa undani kwenye The Interview ya Clouds TV kuanzia namna alivyoingia kwenye matumizi ya madawa ya kulevya, jinsi yalivyomwathiri na namna alivyosaidiwa hadi leo amekuwa hivyo. Ray C alisema aliingia kwenye matumizi ya madawa ya kulevya kutokana na kushawishiwa na aliyekuwa mpenzi wake. “I broke up with my ex , nikasema kwanza nimtoe huyu mtu aliyeniletea balaa hili. Hata mama yangu mwenyewe aliona mabadiliko. I loved him so much with all my heart, but then I had to let him, ilibidi aende cause yeye ndiye aliyeniletea balaa lote.
"So nikasema anyway Mungu naomba unisaidie nampenda huyu kijana lakini hayuko sawa, not for me. We separated, 2010 tukaachana,” alisema. Aliongeza kuwa baada ya kubaki mwenyewe na kujigundua kuwa hayupo sawa alilazimika kujaribu kupigana mwenyewe kuikataa hali hiyo lakini haikuwa rahisi.
“Mbona mimi nilikuwa na bidii sana, mbona nilikuwa very hard working? What’s happening now? Mbona najisikia tu kukaa nyumbani? Mbona mimi nilikuwa nafanya show 10, 20 kwa mwezi lakini sasa hivi hata show moja inanitia uvivu vipi?
"Nikamuomba mwenyezi Mungu anirudishie ile bidii. So what I did nilivyoachana naye, nikasema hebu nitoke nje ya nchi nikajifikirie kwanza mwenyewe kwamba what happened, I have a problem. Hii problem nimeletewa lakini huyo mtu kashatoka sasa unatokaje wewe?
"So nimeenda Nairobi nimekaa tafuta tafuta mahospitali, nikasema I can’t do this alone, I have to go back home. Mama yangu yupo pale and she knows everything.
"Sababu nilikuwa nimeshamwambia ‘Mama mimi nina tatizo hili na hili’. Kalia sana, kaomba sana, nishapelekwa kanisani sana, nshafanyiwa kila kitu lakini nilitakiwa mimi mwenyewe niamue kwamba, this is it, I am ready.”
Ray alisema alipokuwa Nairobi alikuwa akipata fedha nyingi lakini zote zilikuwa zikiishia kwenye madawa ya kulevya.
“Whatever I get inaenda kupotea kwenye starehe hiyo hiyo ambayo haina mbele wala nyuma. Nikipata milioni 2, milioni 5, milioni 10 yote ntakayoipata itaendaaa lakini yote itaisha, kwasababu I was addicted, I was an addict. Vitu vyote vikastop, kwahiyo nikawa nafanya kazi, I became a slave.”
Anasema kuna wakati alikuwa akijishangaa na kujihisi kama si yeye wa zamani na kwamba huenda kulikuwa na mzimu ulioingia mwilini mwake. “Mimi mwenyewe ambaye ndo najijua, nikasema hii si sura yangu, sura yangu ni ile hardworking woman, kuhangaika kutafuta pesa hii sura yangu ya sasa hivi sio, kama nimewekewa mzimu hivi usoni niwe alcoholic mpaka nife ama an addict nife.
Bidii zote nilizopewa na mwenyezi Mungu, baraka zote nilizopewa na mwenyezi Mungu zimeenda. Ni mtu wa kukaa nyumbani kusubiri waniletee, I smoke imeisha the next day ndio hivyo, that was me.”
Leo interview hiyo inaendelea tena Clouds TV
No comments:
Post a Comment