Hatimaye msako wa kocha Jose Mourinho
wa mshambuliaji atakayeongoza safu ya mashambulizi ndani ya kikosi cha
Chelsea umefikia mwisho baada ya klabu hiyo kukamilisha mipango ya
kumsajili mshambuliaji wa kimataifa wa Cameroon Samuel Eto’o Fils .
Eto’o aliingia London usiku wa kuamkia leo kwa usafiri wa treni toka nchini Urusi alikokuwa anaichezea klabu ya Anzhi Makhachkhala ambayo imemruhusu kujiunga na Chelsea kwa usajili wa bure.
Eto’o aliingia London usiku wa kuamkia leo kwa usafiri wa treni toka nchini Urusi alikokuwa anaichezea klabu ya Anzhi Makhachkhala ambayo imemruhusu kujiunga na Chelsea kwa usajili wa bure.
Usajili huo unakuja siku moja baada ya The Blues kuthibitisha kukamilika kwa usajili wa kiungo mshambuliaji Willian ambaye amesajiliwa kwa paundi milioni 30 .
Eto’o anatarajiwa kusaini mkataba wa mwaka moja ndani ya Chelsea ambapo atalipwa paundi milioni 7 kwa mwaka baada ya kufikia makubaliano ya punguzo la mshahara toka paundi milioni 17 kwa mwaka alizokuwa analipwa nchini Urusi ambazo zilimfanya kuwa mchezaji anayelipwa fedha nyingi kuliko wote duniani .
Usajili wa Eto’o unakuja kama mpango mbadala wa Mourinho kusajili mshambuliaji ambaye amekuwa akimtaka baada ya kuthibitisha kumkosa Wayne Rooney wa Manchester United ambaye ameamua kubakia kwenye klabu yake .
Eto’o anaungana na Mourinho kwa mara ya pili baada ya kuchezea kwa mafanikio makubwa wakati wakiwa na Inter Milan ambapo klabu hiyo ya Italia ilitwaa mataji matatu katika msimu wa mwaka 2009/2010 .
No comments:
Post a Comment