Wema Sepetu.
Mwaija Salum na Denis Mtima
DIVA wa filamu za Bongo ambaye
pia ni Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu anasakwa na Jeshi la Polisi
Kituo cha Kawe, Dar es Salaam kwa tuhuma za kufanya fujo hotelini,
kumtukana matusi ya nguoni na kumpiga makofi meneja wa hoteli hiyo,
Godluck Kuyumbu. Songombingo hilo lilijiri saa tano usiku wa Jumatano
iliyopita kwenye hoteli hiyo (jina tunalo) iliyopo Kawe Beach, jijini
Dar.
MAELEZO YA MENEJA
Akizungumza na Ijumaa
Wikienda, meneja huyo alisema siku ya tukio majira ya saa nane mchana,
Wema alifika kwenye mgahawa wa hoteli hiyo akiwa ameongozana na marafiki
zake wapatao kumi.
WEMA, WENZAKE WAZIDIWA NA KILEVI
Meneja huyo akaendelea kusema,
ilipofika saa tano usiku, Wema na marafiki zake walionekana kuzidiwa
na kilevi, wakaanza kufanya fujo kwa kupiga kelele, kitendo
kilichowakera wateja waliokuwa katika mgahawa huo, wengi wakiwa ni
Wazungu ambao waliondoka kutokana na fujo hizo.
Aliongeza kuwa mmoja wa
marafiki wa Wema ambaye ilidaiwa ni mpenzi wake, aliyejulikana kwa jina
moja la D, alichukua glasi na kuipasua chini kwa makusudi huku meneja
huyo akishuhudia.
Meneja akasema: Wakati
wanaondoka, nilimfuata yule jamaa mpaka nje, nikamuuliza ni kwa nini
amevunja glasi kwa makusudi, akanijibu kwa dharau huku akinitukana na
kutishia kunipiga, akawa ananiuliza hiyo glasi ni shilingi ngapi kwani ?.
WEMA AANZA KAZI YA KUSHUSHA KIPIGO
Aliongeza kuwa swali lake kwa
kijana huyo lilionesha kumkera sana Wema, kwani alitoka kwenye gari na
kuanza kumlamba vibao visivyo na idadi meneja huyo huku akimpa maelekezo
kwamba akashitaki popote na hawezi kufanywa kitu kwani yeye ana nguvu
kwenye nchi hii.
“Niliamua kupiga simu Kituo cha Polisi Kawe, wakaja kuangalia mazingira kisha nikaondoka nao kwenda kufungua kesi kituoni.”
Faili la kesi hiyo linasomeka
KW/RB5988/2013, SHAMBULIO. Hadi tunakwenda mitamboni, Wema anasakwa na
polisi ili apandishwe mahakamani.
TUJIKUMBUSHE
Mwaka 2009, Wema alidakwa na
Polisi Kituo cha Magomeni na baadaye kupandishwa katika Mahakama ya
Kinondoni, Dar kwa Hakimu Emilius Mchalu kwa kosa la kuvunja kioo cha
gari la aliyekuwa staa wa filamu Bongo, Marehemu Steven Kanumba chenye
thamani ya shilingi milioni moja.
Hata hivyo, Kanumba aliamua
kuifuta kesi hiyo kwa sababu ya kutaka amani. Wakati huo Wema alikuwa na
uhusiano wa kimapenzi na mjasiriamali aitwaye Jumbe Yusuf Jumbe.
ALIMTISHIA MAISHA BOB JUNIOR
Kama vile haitoshi, mwaka
2011, Wema huyohuyo alilikwaa soo jipya, akakamatwa na Polisi wa
Oysterbay na kufikishwa Mahakama ya Mwanzo, Kinondoni kwa kosa la
kumtusi na kumtishia maisha mwanamuziki wa Bongo Fleva, Rahem Nanji ‘Bob
Junior’.
Katika kesi hiyo, Hakimu
Mariam Masamalo alimtia hatiani Wema na kumhukumu kwenda jela miezi
sita au faini ya shilingi elfu arobaini ambapo alilipa feha hizo. Wakati
huo, Wema alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na Mbongo Fleva, Nasibu
Abdul ‘Diamond’
No comments:
Post a Comment