MATANGAZO

/zest+mkali+3.jpg /TULAMCHA+2+copy.jpg

Wednesday, 10 July 2013

WATU 11 WALIJERUHIWA KATIKA AJALI YA BASI AINA YA TAQWA HUKO MBARALI

Juu na chini ni  Muonekano wa Basi la Kampuni ya   Taqwa baada ya kupata ajali na Watu  11 wamejeruhiwa vibaya baada ya basi  hilo walilokuwa wakisafiria kutoa Jijini Dar es Salaam kwenda Lubambashi nchini Congo DRC kugongana uso kwa uso na lori aina ya Center wilayani Mbarali.



Hapo ni abiria wa Basi hilo la Taqwa wakisubiria Masaada  ili waendelee na safari yao.


  Muonekano wa Basi la Kampuni ya   Taqwa baada ya kupata ajali na Watu  11 wamejeruhiwa vibaya baada ya basi  hilo walilokuwa wakisafiria kutoa Jijini Dar es Salaam kwenda Lubambashi nchini Congo DRC kugongana uso kwa uso na lori aina ya Center wilayani Mbarali.
Watu  11 wamejeruhiwa vibaya baada ya basi la kampuni ya Taqwa walilokuwa wakisafiria kutoa Jijini Dar es Salaam kwenda Lubambashi nchini Congo DRC kugongana uso kwa uso na lori aina ya Center wilayani Mbarali.

Ajali hiyo mbaya ilitokea juzi majira ya saa 2:00 usiku katika mtelemko wa mlima Mambi katika barabara Kuu ya Mbeya –Iringa wilayani Mbarali ikihusisha basi la Kampni ya Taqwa lenye namba za usajili T 396 AXZ na lori aina ya Center lenye namba za usajili T 175 BRA.


Baadhi ya watu walikuwa ndani ya basi hilo walisema kuwa wakati basi hilo likiwa kwenye mwendo mkali katika mteremko huo, lori aina ya Center ambalo lilikuwa likipandisha lilijaribu kupita gari lingine lilikuwa limesimama kando ya barabara, ndipo magari hayo yalipogongana uso kwa uso na kusababisha basi hilo kupoteza mwelekeo na kupinduka mtaroni.


Getruda Kambale ambaye ni raia wa Congo, ni miongoni mwa abiria walionusurika kwenye ajali hiyo ambaye alisema kuwa licha ya basi lao kubondeka vibaya, hakuna mtu aliyepoteza maisha ingawa baadhi ya abiria wameumia vibaya.


“Tunashukuru Mungu hakuna mtu amekufa hapa, lakini dereva wetu ameumia vibaya wamemchukua na kumkimbiza Hospitali,” alisema Kambale.


Alisema wakati yeye akiwa amewa amechoka baada ya kusafiri kwa siku mbili akitokea Nairobi, alishtikia basi likiyumba kasha akasikia kishindo kikubwa na ndipo alijikuta akitolewa kwenye gari hilo kupitia dirishani.


Daktari Msaidizi wa Hospitali ya Misheni Chimala, Peter Seif Kigombola alisema kuwa hospitali hiyo imepokea majeruhi 11, kati yao 10 walikuwa ji abiria wa basi la Taqwa na mmoja alikuwa ni dereva wa lori aina ya Center.


Alisema abiria hao tisa hali zao zinaendelea vizuri, lakini wawili ambao ni dereva wa basin a kondakta wake hali zao ni mbaya na kuwa wamepewa rufaa ya kwenda katika Hospitali ya Rufaa Mbeya kwa matibabu zaidi.


Alisema kuwa dereva na kondakta wake walivunjika viungo mbalimbali vya miili yao kama vile mikono na miguu na kupata majeraha mengine kichwani, hali ambayo imesababisha hali zao kuwa mbaya.


Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya, Barakael Masaki amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema kuwa bado Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi wa ajali hiyo pamoja na  kukusanya taarifa za majeruhi na kuwa atatoa taarifa ya ajali hiyo baadaye.

No comments:

Post a Comment