Profesa J akiwa na mama yake mzazi Bi Rosemary Majanjara Haule enzi za uhai wake. Picha hii ilipigwa April 4, 2008 katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam wakati wa sherehe ya uzinduzi wa albamu mpya ya Profesa J ya 'Aluta Continua'
HABARI
ZILIZOPOKEWA USIKU HUU NI KWAMBA MAMA YAKE MZAZI MSANII MAARUFU WA
MUZIKI NCHINI, JOSEPH HAULE A.KA. 'PROFESA J' AMEFARIKI DUNIA USIKU HUU
BAADA YA KUGONGWA NA GARI MAENEO YA MBEZI JUU, JIJINI DAR ES SALAAM,
ALIKOKUWA ANAISHI NA MWANAE.
HABARI
ZINASEMA MAREHEMU, BI. ROSEMARY MAJANJARA HAULE, ALIGONGWA NA GARI
AKIWA ANAVUKA BARABARA KUELEKEA DUKANI KIASI CHA SAA MBILI USIKU, NA
KWAMBA BAADA YA KUGONGWA WASAMARIA WEMA WALIMKIBIZA HOSPITALINI TUMBI
KWA KUTUMIA BAJAJI AMBAKO ALIFARIKI DUNIA. TAARIFA ZA AWALI HAZIJATAJA
AINA YA GARI NA KAMA BAADA YA AJALI HIYO LILISIMAMA AU LA.
PROFESA
J AMETHIBITISHA HILO MUDA MFUPI ULIOPITA, NA KUSEMA INAMUIA VIGUMU
KUAMINI IMETOKEA KWANI ANASEMA MAREHEMU MNAMO SAA MBILI HIVI ALIMPIGIA
SIMU NA KUMWELEZA KUWA AMEPATA AJALI NA KWAMBA WAKATI HUO YUKO KITUO CHA
POLISI, BILA SHAKA KUPATA FOMU YA PF 3 YA KUMUWEZESHA KWENDA KUTIBIWA
HOSPITALI.
"MAMA
ALINIAMBIA MWANANGU NIMEGONGWA NA GARI....NJOO NIKO POLISI
NAANDIKISHA....MWANANGU NAKUFA....ALINIAMBIA MAMA NA MARA SIMU
IKAKATIKA. KILA NILIPOJARIBU KUPIGA IKAWA HAIPATIKANI..." ALISEMA
PROFESA J KWA UCHUNGU.
ANASEMA
WAKATI ANAPIGIWA SIMU NA MAMA YAKE YEYE ALIKUWA KATIKA MGAHAWA WA
NYUMBANI LOUNGE, NAMANGA, DAR ES SALAAM, ALIKOKUWA KATIKA KIKAO NA LADY
JAY DEE NA MUMEWE GADNA G. HABASH, AMBAO BAADA YA TAARIFA HIYO
WALIMSINDIKIZA HADI HOSPITALI YA TUMBI.
"TULIPOFIKA
HOSPITALI SIKUAMINI KUONA BADALA YA KUPELEKWA WODINI AMBAKO NILIDHANI
MAMA ATAKUWA AMELAZWA NIKAPELEKWA CHUMBA CHA MAITI AMBAKO NILIMKUTA MAMA
AKIWA MAREHEMU", ALISEMA PROFESA J KWA MAJONZI.
GLOBU
YA JAMII INATOA MKONO WA POLE KWA PROFESA J KWA MSIBA HUU MZITO NA WA
KUSIKITISHA. TUNAMWOMBA MOLA AMPE NGUVU YEYE NA FAMILIA YAKE KATIKA
WAKATI HUU MGUMU.
TUTAENDELEA
KUWAPASHA KINACHOJIRI KADRI HABARI ZAIDI ZITAPOPATIKANA. KWA SASA
PROFESA J NA WADAU WENGINE WAKO NYUMBANI KWAKE MBEZI JUU.
source-tzdailyeye
No comments:
Post a Comment