Wanajeshi wa Brigedi Maalum wakiwa katika mazoezi makali
yaliyofanyika hivi karibuni huko Goma Mashariki ya Demokrasia ya
Kongo
Mmoja wa walinda amani kupitia Brigedi Maalum inayoundwa na
wanajeshi kutoka Tanzania, Afrika ya Kusini na Malawi akiwa katika
moja ya mazoezi yaliyofanyika hivi karibu huko Goma. Kamanda Mkuu wa
Misheni ya Kulinda Amani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, (
MONUSCO ) Luteni Jenerali Carlos Albeto dos Santos Cruz ametakanza jana
jumanne akiwa Goma kwamba MONUSCO itaanza rasmi kuitumia Brigedi
Maalum na ametoa saa 48 kuanzia saa kumi jioni kwa saa za Goma jana
siku ya Jumanne waasi wote kusalimisha silaha zao, na kwamba ifikapo
saa kumi jioni kwa saa za Goma siku ya Alhamisi Agosti Mosi wale wote
ambao watakuwa hawajasalimisha silaha zao watachukuliwa kama tishio
la usalama kwa wananchi na MONUSCO italazimika kuwapokonya ikiwa ni
pamoja na kutumia nguvu kwa mujibu wa Mamlaka iliyopewa na Sheria
zinazowaruhusu kufanya hivyo.
Na
Mwandishi Maalum
Misheni ya Kutuliza
Amani katika Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo ( MONUSCO)
imetangaza kwamba kwa mara ya kwanza
itaanza kuitumia Brigedi Maalum ( Force Intervention Brigade)
katika kudhibiti eneo maalum la usalama
( security zone ) kuzunguka mji
wa Goma ulioko Mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na imewapa saa 48 waasi kusalimisha silaha zao.
Taarifa
iliyotolewa na
MONUSCO na kusambazwa na Idara
ya Mawasiliano ya Umoja wa Mataifa
jana jumanne, inaeleza kwamba watu binafsi katika eneo la Kivu ya
Magharibi ambalo linajumisha Goma
na Sake
na ambao hawahusiki na vyombo vya usalama watapewa saa 48 kuanzia saa
kumi jana kwa saa za Goma ( Jumanne ) kuzisalimisha silaha zao katika
Misheni hiyo na kujiunga na mchakato wa DDR/RR unaoratibu
upokonyaji, usambaratishaji, urejeshwaji
makwao, kuwaunganisha na jamii na
kuwapatia makazi.
Baada ya saa kumi jioni ya
Alhamisi, Agosti Mosi. Taarifa hiyo inasema. Wale wote ambao watakuwa
hawajasalimisha silaha zao watachukuliwa kama
tishio kwa usalama wa wananchi na
MONUSCO itachukua hatua zote muhimu kuwapokonya silaha hizo ikiwa ni
pamoja na kutumia nguvu kama
ilivyoainishwa katika Mamlaka na sheria za
ushiriki za MONOSCO.
Kwa
mujibu wa taarifa hiyo zaidi ya wananchi milioni
moja wanaishi katika eneo dogo la Goma na Sake na kando kando ya
barabara ambayo inawaunganisha na kambi ya wakimbizi ya Mugungu
ambayo ni makazi ya
muda ya watu karibu 70, 000 ambao
wameyakimbia makazi yao kutokana na mapigano.
Kwa mujibu wa MONUSCO, tangu kati kati ya mwezi Mei
eneo hilo limeshuhudia mapigano ya mara kwa mara kutoka kwa kundi la M23 dhidi
ya majeshi ya Serikali ya
FARDC ikiwa ni jaribio la wazi la kutaka kusonga mbele kuelekea Goma na Sake.
“ Katika mashambulizi hayo, likiwamo la hivi karibuni
la Julai 14, M23 walitumia kiholela
silaha zao za moto zikiwamo silaha nzito ambazo zimesababisha wananchi kujeruhiwa” .
Taarifa hiyo imeongeza kwamba kundi
hilo la M23 katika mashambulizi hayo limelenga pia Vituo vya Umoja wa Mataifa.
Aidha taarifa
hiyo inabainisha kwamba eneo hilo maalum
la usalama ( security zone) litasaidia
kudhibiti tishio la moja kwa moja mbali
na eneo la nje ya Goma na pengine eneo hilo linaweza kupanuliwa na kurudiwa
sehemu nyingine kutakako hitajika.
Tamko
hilo la kutoa saa 48 kwa waasi kusalimisha silaha
zao linafuatia kuwasili katika eneo la Goma kwa Kamanda Mkuu wa
MONUSCO, Luteni Jenerali Carlos Alberto dos Santos Cruz, ambaye
alitangaza kwamba Misheni ya MONUSCO
itaunga mkono jeshi la Serikali (
FARDC) katika kuanzisha eneo la usalama
kuzunguma eneo la Goma na vitongoji vyake.
Taarifa hiyo inamkariri Kamanda Mkuu wa MONUSCO akiyapongeza majeshi ya serikali kwa
kazi nzuri iliyofanya wiki
iliyopita ya kuwadhibiti M23. Ingawa
anasema eneo la Goma na Sake bado
limo katika mazingira magumu sana na kwamba ni wajibu wa wahusika wote
kuhakikisha wahalifu wote hawaendelei kuhatarisha raia wa eneo hilo.
Kwa
mwaka
uliopitia , kundi la M23 pamoja na makundi mengine yenye silaha yamekuwa
yakipambana mara kwa mara na majeshi ya serikali katika Mashariki ya
Kongo, huku makundi hayo yenye silaha mwezi Novemba mwaka jana
yakiikalia Goma kwa muda.
Aidha mapingano ya hivi karibuni ambayo safari hii yalihusisha pia kundi
jingine la wanagambo wenye silaha lenye
asili yake nchini Uganda, yamesababisha zaidi ya wananchi 100,000 kuyakimbia makazi yao na hivyo kuongeza
mgogoro wa kibinadamu katika eneo hilo
linalohusisha watu wengine 2.6 milioni ambao wameyakimbia makazi yao huku
wengine 6.4 milioni wakihitaji chakula
na huduma za dharura.
Wakati huo huo,
Kaimu Mkuu wa MONUSCO Bw. Moustapha Soumare katika taarifa yake ametoa wito kwa pande zote kutafuta
suluhu ya kisiasa kwa matatizo ya
DRC kupitia Mpango Mpana wa Kisiasa wa Umoja wa Mataifa kuhusu amani,
usalama na ushirikiano wa maendeleo katika DRC na eneo la Maziwa Makuu uliopitisha mwezi wa Februari na
viongozi 11 wa Afrika na Taasisi nne
za Kikanda na Kimataifa.
Aidha akasema
katika kipindi hiki ambacho
suluhu la kisiasa linatafutwa MONUSCO itatumia nguvu iliyonayo kuwalinda
wananchi dhidi ya hatari zitokanazo na
makundi ya waasi.
No comments:
Post a Comment