Mcheza kiungo wa Barcelona Cesc Fabregas amesema hana nia yoyote ya kuihama klabu hiyo na kurejea tena nchini England.
Hayo ni kwa mujibu wa kocha wake Tito Vilanova.
Klabu
ya Manchester United siku ya Jumatatu iliwasilisha ombi la kutaka
kumasajili nahodha huyo wa zamani wa Arsenal, kwa kitita cha pauni
milioni ishirini na tano, lakini Vilanova amesema mchezaji huyo anataka
kusalia nchini Uhispania kwa sasa.
''Ni ishara nzuri kwa klabu yoyote kupata maombi
kutoka kwa vilabu vingine, vinavyotaka kuwasajili wachezaji wake,
lakini Fabregas amesema anataka kusalia'' Alisema kocha huyo.
Vilanova ameongeza kusema kuwa'' Fabregas hataki
kujiunga na timu zingine kwa sababu ya pesa au kutokana na muda wake wa
kucheza uliosalia.
Anafahamu huku kuna ushindani mkali, lakini ni
uamuzi wake kusalia na Barcelona. Kwa sasa nimetulia''.
Kufikia sasa Barcelona halijasema lolote rasmi
kuhusiana na ombi hilo la Manchester United, ambalo linaaminika kuwa
chini ya dhamana kamili ya mchezaji huyo.
Fabregas alikuwa mchezaji mchanga zaidi wa
Arsenal wakakti aliocheza dhidi ya Rotherham United wakati wa mechi ya
kombe la ligi mwaka wa 2003 akiwa na miaka kumi na saba na siku mia moja
na sabini na saba.
Alikuwa miongoni mwa wachezaji wa Arsenal
walioishinda timu ya Manchester United kupitia mikwaju ya penalti kwa
fainali ya kombe la FA mwaka wa 2005.
Vile vile Fabregas, anaichezea timu ya taifa ya
Uhispania na aliisaidia kunyakua kombe la dunia na pia kuwa mabingwa wa
bara Ulaya mara mbili.
Alijiunga na Arsenal mwaka wa 2003 akiwa na umri wa miaka kumi na sita.
Fabregas aliichezea Arsenal mechi 303 na kufunga
magoli 57, kabla ya kusajiliwa na Barcelona kwa kitita cha pauni
milioni 25.4 kwa mkataba wa miaka mitano kwa wa 2011
No comments:
Post a Comment