Hali imekuwa ni tofauti kidogo kwa mwanafunzi wa chuo kimoja hapa nchini ambaye yuko mwaka wa kwanza na anategemea kuingia mwaka wa pili.
Akiongea na mtandao huu kwa sharti la kutotajwa jina , mwanafunzi huyo amefunguka na kudai kuwa Exile imemuathiri sana kisaikolojia.Imemfanya aishi kama mtumwa huku taaluma yake ikiyumba kwa kasi.
Hili ni simulizi la mwanafunzi huyo:
"Maisha ya shule yana changamoto nyingi sana.Kwa mtu yeyote ambaye ni mcha mungu ni lazima itamuwia vigumu sana kukabiliana na hali hii.
"Nasema hivi kwa sababu ndani ya hosteli huwa tunaishi watu tofauti wenye malezi tofauti.Kasheshe ni kwetu sisi first year...
"Mazingira kwetu ni mageni na ndani ya hosteli tunaishi na mabraza wa miaka ya juu wenye wapenzi wao hapo hapo chuoni ambao huwaleta vyumbani na wakati mwngine hulala nao.
"Wanapokuja na wapenzi wao vyumbani ni lazima uwapishe wafanye mambo yao.Na ukiwapisha maana yake utoke kwa zaidi ya masaa matatu mpaka matano
"Ndani ya chumba changu tulikuwa tunaishi watatu, mmoja mwaka wa pili, mwingine wa tatu na mimi mwaka wa kwanza.Wote hao walikuwa na wapenzi wao hapo hapo chuoni.
"Siku zote za wikiendi walikuwa wamezigawana.Mmmoja ilikuwa ni jumamosi na mwingine jumapili.Yaani kwa kifupi ni kwamba sikuwa na uhuru wa kukaa chumbani siku za wikiendi na wakati mwingine hata siku za wiki.
"Nimeamua niwe muwazi maana hali hii imekuwa ni kero kwangu na imekuwa ikiniathiri sana kisaikilojia na kusababisha taaluma yangu iyumbe nikilinganisha na nilipokuwa naanza.
"Naomba nitoe ombi kwa wanafunzi wenzangu.Sote tuko vyuoni kutafuta maisha na zile hosteli tunazilipia kwa gharama sawa.Kwa nini umsumbue mwenzako wakati gesti zipo?..Yangu ni hayo tu
No comments:
Post a Comment