Kutoka
kushoto ni Tatu Issa mwanafunzi wa chuo kikuu cha SAUTI tawi la Songea,
Tamimu Adam mtangazaji wa Radio Jogoo FM na Aneth Mponda mwanafunzi wa
chuo kikuu cha SAUTI tawi la songea wakiwa wanajadili mada inayohusu
matumizi ya mitaandao ya kijamii katika kipindi cha Jamvi letu
kinachoendesha na kituo hicho cha radio katika manispaa ya songea Mkoani
Ruvuma '
Aneth
akielezea faida anayoipata kupitia mitandao ya kijamii hasa Facebook
ambayo kwake ni rahisi kutumia ikiwa ni kubadilishana mawazo ila kwa
upande wa Twitter kwake inamuwia ngumu kuitumia kutokana na ilivyo, kwa
upande wa changamoto anazokutana nazo amesema "kuna watu humu katika
mitandao hutumia sivyo mara kwa mara unakuta wanakutaka kimapenzi na
ukimkatalia bado hakomi kila akikuona upo hewani lazima akutumie ujumbe
wa mapenzi wakati umemkatalia yeye anakung'ang'nia pia kuna baadhi
huweka picha za ngono amabazo ni kinyume na maadili ya kiTanzania
unakuta ni mtu mzima na haendani na matendo anayoyafanya pia kuana
wengine hawajiamini wanaweka picha si zao "alisema.
Tamimu Adam akisikiliza kwa makini mawazo toka kwa washiriki wa kipindi cha Jamvi letu
Tatu
Issa akielezea faida ya matumizi ya mitandao ya kijamii kwa upande wake
ni kupata taarifa mbalimbali pia kubadilishana mawazo na marafiki mbali
mabali na kupata marafiki kupitia mitaandao pia kwa siku anasema
anaingia mara mbili na hutumia zaidi ya masaa matatu na moja ya mtandao
anaopenda ni facebook.
"Japo
natumia mitandao hii ya kijamii lakini bado siiyamini kwani kuna baadhi
huweka habari zisizo za ukweli mfano kuhusu mitandao ya kijamii
iliyozusha juu ya kifo cha msanii Saida kaloli" alisema
ukweli ni huo kila ktu kina faida na hasara zake
ReplyDelete