Askari saba wa Jeshi la Ulinzi la
Wananchi wa Tanzania (JWTZ), waliouawa katika jimbo la Darfur nchini
Sudan, wanatarajiwa kuagwa leo kwenye viwanja vya makao makuu ya jeshi
hilo.
Miili ya
wanajeshi hao iliwasili nchini juzi kwa ndege maalumu katika Uwanja wa
Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu J. K Nyerere, Terminal One na kwenda
kuhifadhiwa kwenye Hospitali ya Rufaa ya Lugalo jijini Dar es Salaam.Wanajeshi
waliouawa ni Sajenti Shaibu Othuman, Koplo Oswald Chaula, Koplo Mohamed
Juma, Koplo Mohamed Chikilizo, Rodney Ndunguru, Peter Werema na
Fortunatus Msofe.
Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana na Kurugenzi ya Habari na Uhusiano, Makao Makuu ya JWTZ, ilieleza kuwa askari hao wataagwa leo na shughuli hiyo itahudhuriwa na familia, makamanda wa jeshi na viongozi wa Serikali.
“Shughuli ya kuaga kwa heshima za kijeshi itaanza saa tatu kamili asubuhi katika viwanja vya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Upanga na itaendelea mpaka mchana kabla ya kusafirishwa,” ilisema taarifa hiyo.
Wanajeshi hao ambao ni miongoni mwa askari wa kikosi cha Umoja wa Mataifa cha Kulinda Amani katika Jimbo la Darfur nchini Sudan, waliuawa kutokana na mashambulizi ya kushtukiza yaliyofanywa na waasi wanaopigana na Serikali, hivyo kuwa ni mara ya kwanza kwa idadi kubwa ya wanajeshi wa Tanzania wanaolinda amani katika nchi mbalimbali kuuawa kwa wakati mmoja.

No comments:
Post a Comment