MATANGAZO

/zest+mkali+3.jpg /TULAMCHA+2+copy.jpg

Wednesday, 10 July 2013

HATIMAYE CHAMA CHA MUSLIM BROTHERHOOD CHAPINGA VIKALI RATIBA YA UCHAGUZI MKUU NCHINI MISRI



Maafisa wakuu wa chama cha Muslim Brotherhood, wamepinga vikali pendekezo la rais wa mpito Adly Mansour kuweka ratiba ya kuandaa uchaguzi mkuu mwaka ujao.
Mmoja wa viongozi wa chama hicho, Essam al-Erian anasema kuwa mpango huo utakaojumuisha mabadiliko ya kikatiba na kura mwaka ujao unarejesha nchi hiyo ilipokuwa baada ya mapinduzi ya kumwondoa mamlakani Hosni Mubarak. 

Rais wa mpito alitangaza kuwa uchaguzi utafanyika mwaka ujao katika juhudi zake za kutuliza maandamano na hali ya taharuki nchini humo.

Tangazo hilo lilitolewa wakati mgogoro ukizidi kati ya jeshi na wafuasi wa rais aliyepinduliwa Mohammed Morsi kar
ibu na kambi ya jeshi mjini Cairo ambako zaidi ya watu 50 waliuawa hapo jana wakati wa mapigano na wanajeshi.

Aidha tangazo la Rais Adly Mansour, linaashiria mageuzi katika katiba kwa kuitisha kura ya maoni ambayo huenda ikachangia kufanyika kwa uchaguzi mwaka ujao.

Hii inakuja wakati ambapo watu 51 wamethibitishwa kuuawa mjini Cairo.

Chama cha Muslim Brotherhood kinasema kuwa wanachama wake walipigwa risasi wakati walipokuwa wanakesha nje ya makano ambapo Morsi anazuiliwa, lakini jeshi linasema liliwafyatulia risasi kwani waandamanaji nao walikuwa wamejihami.

Rais Morsi, aliyekuwa rais wa kiisilamu na wa kwanza kuchaguliwa kidemokrasia, aliondolewa mamlakani na jeshi wiki jana baada ya maandamano makubwa ya kumpinga kufanyika.

Wafuasi wake wanatuhumu jeshi kwa kufanya mapinduzi, lakini wapinzani wake wanasema hatua hiyo ni mwendelezo wa mapinduzi yaliyomwondoa mamlakani aliyekuwa rais Hosni Mubarak mwaka 2011.

Bwana Mansour alitoa amri hiyo Jumatatu jioni.

Amri hiyo inasema kuwa jopo la kufanyia katiba marekebisho ambalo lilifutwa kazi wiki jana, litaundwa tena katika kipindi cha siku 15.

Mabadiliko hayo kisha yatapigiwa kura ya maoni. Mchakato utapangwa kufanyika katika muda wa miezi minne.

Baada ya kura ya maoni , uchaguzi wa wabunge huenda ukafanyika mapema mwaka 2014.

Hatimaye uchaguzi utafanyika punde baada ya bunge jipya kuundwa.

BBC

No comments:

Post a Comment