BAADA
ya kukamatwa na dawa za kulevya nchini Afrika Kusini, msanii
anayeshiriki katika video za wasanii wa muziki wa bongo fleva, Agnes
Jerald 'Masogange' na mwenzake Melisa Edward, ukweli umeibainika kwamba
dawa walizokamatwa nazo ni za kutengenezea dawa za kulevya, ambazo
hazipatikani nchini na hazina matumizi yoyote.
Kupitia
taarifa rasmi zilionesha kuwa, Chemical bashirifu ndiyo aina ya dawa
walizokamatwa nazo nchini humo, ambapo wasanii hao walikamatwa nchini
Afrika Kusini wakitokea Tanzania.
Akizungumza
ofisini kwake Dar es Salaam leo Kamishina wa Tume ya Kuratibu na
Kuthibiti Dawa za Kulevya nchini, Christopher Shekiondo alisema kwamba
kwa mujibu wa sheria za nchi, dawa walizo kamatwanazo wasichana hao
zinatumika kutengenezea dawa za kulevya, ambapo adhabu yao ni sawa na
mtu aliyekamatwa na dawa za kulevya.
Wasichana
hao walikamatwa Julai 5, mwaka huu nchini humo wakiwa shehena ya dawa
za kulevya zenye thamani ya sh. bilioni 6.8 wakitokea Tanzania.
Shekiondo alisema dawa walizokamatwa nazo
hazitumiki moja kwa moja kama dawa, bali zinatumika kutengenezea dawa
za kulevya hivyo kwa mujibu wa sheria, adhabu zao zinakwenda sambamba na
waliokamtwa na dawa za kulevya.
"Dawa
hizo hazitumiki moja kwa moja bali zinatumika kutengenezea dawa za
kulevya, hivyo kama taarifa tulizopata ni sahihi juu ya aina ya dawa
walizokamatwa nazo na dawa hizi hazitumiki sana nchini, bali zinatumika
Afrika Kusini, Asia pamoja na Ulaya," alisema Shekiondo.
Alisema kwa mujibu wa sheria za nchi, mtu anayekamatwa na dawa hizo mara nyingi hukumbwa na adhabu ya kuhukumiwa miaka 20 au kifungo cha maisha.
Alisema kwa mujibu wa sheria za nchi, mtu anayekamatwa na dawa hizo mara nyingi hukumbwa na adhabu ya kuhukumiwa miaka 20 au kifungo cha maisha.
Akielezea
kuhusu wasichana hao wawili kupanda kizimbana juzi, Kamishina huyo
aliweka wazi kuwa hadi sasa hawajapata taarifa zozote rasmi, zaidi ya
kupokea zile za awali za kushikiriwa na Jeshi la Polisi Afrika Kusini
kwa ajili ya uchunguzi.
Kamishina
huyo alisema inaonesha Watanzania wengi wamekamatwa na dawa za kulevya
nchini Brazil ambao idadi yao inafikia 109, ambapo wengi wao
wameshahukumiwa.
Alisema
watu hao wamekamtwa nchini humo, wakiwa na dawa aina ya cocain kwa
ajili ya kusafirisha nchi nyingine, huku baadhi yao wamehukumiwa
kunyongwa pamoja na kifungo cha maisha, ingawa idadi kamili ya watu hao
bado haijafika rasmi.
"Tumepokea
taarifa jumla ya Watanzania 109 wamekamtwa nchini Brazil, ingawa bado
tunasubiri kujua ni wangapi waliohukumiwa kifo, pamoja na kifungo cha
maisha," alisema Shekiondo.
Aliongezea
kuwa baadhi ya nchi nyingine, ambazo Watanzania wanakamatwa na dawa
hizo za kulevya wakiwa wanasafirisha ni China vijana 34, Kenya 30,
Pakistani 16, Falme za Kiarabu ikiwemo Dubai 14, pamoja na nchi
nyingine kama Japan, Argentina, Msumbiji, Afrika Kusini, Ureno, pamoja
na Uingereza.
Akizungumzia
hukumu ambazo zimeshatolewa baadhi ya nchi walizokamatwa Watanzania
hao,, Kamishina huyo alisema Brazil ambayo ndiyo Watanzania wengi
wamekamatwa idadi kamili, bado hawajapata ingawa Kenya tayari wapo
waliohukumiwa kifungo cha maisha, huku wengine wakiwa wamehukumiwa
kifungo cha miaka 20 hadi 40, nchi China wapo waliohukumiwa kifo na
kifungo cha maisha.
Shekiondo alisema Tanzania kwa sasa inajulikana kama ni njia ya kusafirisha dawa hizo.
Shekiondo alisema Tanzania kwa sasa inajulikana kama ni njia ya kusafirisha dawa hizo.
Alisema
kuna baadhi ya watu wanatumia maji kusafirisha dawa hizo, yaani meli,
jahazi pamoja na mitumbwi, hivyo wana mikakati ya kutoa elimu kwa jamii
kuhusu udhibiti wa matumizi ya dawa za kulevya.
No comments:
Post a Comment