Aunty
Lulu alinaswa na paparazi wetu maeneo ya Kinondoni, Jumatatu (siku
ambayo Obama aliwasili) ambapo alionekana akipiga simu kwa rafiki zake
wanaofanya kazi ikulu akiwaomba japo kitambulisho cha kuingia kwenye
mkutano aliohutubia rais huyo.
Akizungumza na paparazi wetu Aunty Lulu alisema tangu aliposikia taarifa za ujio wa Obama Tanzania, alifurahi na alikuwa akimuota kila mara kwani huwa akisikia sauti yake akiwa anahutubia anachanganyikiwa ndiyo maana alifanya kila jitihada za kuingia ikulu lakini ilishindikana.

“Jamani serikali ingetuangalia hata sisi jamani tumuone Obama naye atuone sisi wasichana wa Kitanzania tulivyo wazuri, warembo na wakarimu, wageni wengi wakiingia Bongo lazima warudi kwa mara nyingine!” alisema msanii huyo.
chanzo:globalpublishers
No comments:
Post a Comment