MATANGAZO

/zest+mkali+3.jpg /TULAMCHA+2+copy.jpg

Wednesday 10 July 2013

AUNT LULU AFUNGUKA ADAI HAYUPO TAYARI TENA KUMVULIA NGUO MR. BOND,SOMA ZAID

Mwigizaji  wa sinema za Kibongo, Lulu Mathias Semagongo ‘Aunty Lulu’ amesema yeye na aliyekuwa mpenzi wake, Bond Bin Salim imebaki historia na kamwe hawawezi kurudiana naye  japo  anayajua  mapenzi.

Akizungumza na mwandishi  wetu hivi karibuni, Aunty Lulu alisema ameshaamua kujituliza  kwa  mpenzi wake wa sasa  hivyo hata iweje hawezi kurudiana na Bond.
 
“Jamani kwa sasa mnaona nimebadili kabisa staili ya maisha yangu hivyo Bond atabaki kuwa rafiki kama walivyo marafiki zangu wengine.
 
“Niliwahi kuachana naye kipindi flani baadaye tukarudiana kutokana  na ukweli  kwamba  ni  mwanaume  anayejua  kupenda  na  anayajua  mapenzi ,lakini hii ya sasa ndiyo imetoka, kamwe siwezi kurudiana naye,” alisema Aunty Lulu.

No comments:

Post a Comment