Mtandao wa bongo movies umetumiwa madai, kumhusu mwanadada muigizaji wa Filamu aliyepata tuzo
hivi karibuni, Jennifer Kyaka anakwenda na jina la kisanii la Odama kuhusu safari zake za kwenda nje ya nchi.
Habari au tuhuma hizi , zinasema kuwa
mwanadada huyo huwa
haendi nje ya nchi kama anavyowaambia washabiki wake kupitia blog yake
ya odama1.blogspot.com
kuwa anasafiri kwenda nje kikazi zaidi, na badala yake imesemwa kuwa
huwa anabaki hapa hapa nchini akijifanya yupo nje ya nchi,akiwa na lengo
la
kutafuta kulazimisha umaarufu
ushahidi wa picha mbalimbali toka kwenye mtandao mmoja wa kijamii ambao staa huyo Mdau aliyepeleka tuhuma hizo, amesema kuwa ana ushahidi wa kutosha na katuma anautumia kudanganya zikimuonesha akiwa maeneo mbalimbali ya “duniani huko” ambayo kwa kuangalia picha hizo anasema kuwa ni feki na zimetengenezwa kwa kutumia teknolojia tu ya kuhariri picha maarufu kama “PHOTOSHOP”Mtandao wa Bongo Movies umewaomba wadau wenye majibu na utaalamu wa picha wasaidie kwa kutazama picha hizi ili kuthibitisha kama tuhuma hii ina ukweli wowote.
No comments:
Post a Comment