Hatimaye jana usiku timu nne zitakazocheza nusu fainali ya kombe la
mabara zimejulikana kwa Spain kuikanya 3-0 Nigeria huku Uruguay nao
wakijipigia 8-0 Tahiti. Hizi zifuatazo ndio takwimu zilizotengenezwa
kupitia michezo hiyo.
- Spain jana usiku wameweka rekodi ya kutokufungwa kwenye 28 za
mashindano, hii ni rekodi mpya wakiivunja ile ya mechi 27 iliyowekwa na
Ufaransa.
- Timu zote zilizoingia kwenye nusu fainali ya kombe la mabara - tayari wameshawahi kubeba ubingwa wa kombe la dunia.
- Spain wameweza kufunga katika mechi ya 15 mfululizo.
- Mabao manne ya mshambuliaji wa Uruguay - Hernandez, yamemfanya awe
mchezaji wa nne kufunga mabao manne katika historia ya kombe la mabara.
- Fernando Torres sasa amefunga jumla ya mabao 8 katika historia ya
kombe la mabara, amebakiza bao moja kufikia rekodi ya wafungaji bora wa
muda wote wa michuano hiyo Ronaldinho na Cuauhtemoc Blanco wenye mabao 9
kila mmoja.
- Ushindi wa Uruguay wa 8-0 dhidi ya Tahiti, umeifikia rekodi yao ya
ushindi mkubwa kabisa katika michuano ya FIFA (1950 FIFA World Cup v
Bolivia)
- Luis Suarez sasa ametimiza mabao 36 akiwa na jezi ya Uruguay, hivyo
kujiwekea rekodi ya kuwa mfungaji bora wa muda wote wa timu ya taifa ya
Uruguay - akimfunika Diego Forlan mwenye mabao 35.
chanzo-shafiidauda.com
No comments:
Post a Comment