WAKATI Serikali ya Tanzania ikiendelea na maandalizi ya kupokea msafara wa watu 700 waliotarajia kuingia nchini kwa ziara ya Rais wa Marekani Barack Obama, Rais huyo amesitisha safari yake.
Ikulu ya Marekani imetangaza kwamba msafara wa Rais Obama kuja kutembelea Bara la Afrika haitakuwepo tena,baada ya serikali ya nchi hiyo kukosa fedha itakayoweza kugaramia safari ya Rais huyo.
Taarifa iliyonaswa na kutoka katika
mitandao mbalimnali nchini Uingereza na Marekani zinaeleza kwamba
mbali na suala la bajeti ya Rais huyo kuja nchini Tanzania kuwa kubwa
pia kamati ya sheria ,ulinzi na usalama wa Marekani imeshindwa
kuthibitisha juu ya suala la ulinzi na Usalama wa Rais Obama katika
kipindi chote atakachokuwa nchini Tanzania pamoja na baadhi ya nchi
Barani Afrika.
Taarifa hiyo pia ilieleza kwamba msafara wa Rais Obama unahitaji
maandalizi ya kutosha kwa sababu ni msafara unaohusisha watu wengi
pamoja na vyombo mbalimbali vya ulinzi ikiwemo wanyama.
Msemaji wa Ikulu ya Marekani alisema kwamba serikali ilijaribu
kuangalia uwezekano wa Rais Obama kuja Tanzania na baadaye kutembelea
Senegel pamoja na Afrika Kusini ambapo alitakiwa kukaa Tanzania kwa saa
mbili tu lakini gharama za ulinzi imekuwa kubwa sana.
Katika msafara wa Obama inatakiwa kuwe na ndege mbili za mwendo kasi,
kwa ajili ya kulinda ndege ya Rais,iwepo ndege za askari wa majini
zinazotembea kwenye meli habarini, iwepo pea maalum za magari zitakazo
sushwa katika nchi zote tatu mapema kwa kutumia ndege za jeshi kwa ajili
kuimarisha ulinzi kabla ya Rais kutua katika nchi hizo" alisema Mseaji
wa Ikulu ya marekani Josh Earnest.
Nakala ya taarifa hiyo
pia ilimkariri msemaji huyo wa Ikulu ya Marekani akisema kwamba pia
katika msafari huo ni lazima iwe na vifaa maalum vya kutolea matibabu
katika kipindi chote cha ziara ya Rais, lazima pia iwe na chombo maalum
kwa ajili ya waandishi mbalimbali wa habari pamoja na vyombo vingine vya
usalama kwa ajili ya kutoa taarifa ya safari ya Rais ,pamoja ndege
zitakazokuwa zikizunguka kuangalia hali ya usalama katika hoteli zote
atakapo kuwa ana alala Rais Obama na msafara wake.
Taarifa hiyo ilifafanua kwamba safari hiyo ndiyo safari kubwa kuliko
aliyowahi kuifanya Barani Afrika ambapo alifika nchini Ghana, tangu
alipochaguliwa kuwa Rais wa Marekani mwaka 2009 ambapo inakadiriwa kuwa
itachukua kati ya dola za marekani 60 million sawa na tsh bilioni
96,000,000,000 na dola 100 milion sawa tsh bilioni 160,000,000,000.
Read more: http://talkbongo.blogspot.com/2013/06/breaking-newzz-rais-obama-ahairisha.html#ixzz2WDlkk8r1
No comments:
Post a Comment