MATANGAZO

/zest+mkali+3.jpg /TULAMCHA+2+copy.jpg

Wednesday 19 June 2013

POLISI ADAIWA KUUA RAIA MBOZI



TAARIFA zilizofika kwenye chumba chetu cha habari kwenye kalulunga blog, kutoka eneo la Njia panda Iyula wilaya ya Mbozi mkoani Mbeya, zimesema kuwa barabara kuu ya Mbeya Zambia imefungwa na wananchi baada ya mmoja wao kudaiwa kupigwa risasi na askari polisi.

Mwananchi aliyepo eneo la tukio, amesema kuwa wananchi walikuwa kwenye mkutano nwa hadhara, ndipo wakajitokeza askari na kuzingira nyumba ya mwanakijiji mmoja aliyekuwa eneo la mkutano hali iliyomlazimu kuinuka na kwenda kuwauliza kulikoni hali ambayo ikazunka sintofahamu kisha risasi kuanza kurushwa na hatimaye mwananchi huyo kugundulika kuwa amefariki.

Taarifa zaidi tutaendelea kuwaletea...

No comments:

Post a Comment