MATANGAZO

/zest+mkali+3.jpg /TULAMCHA+2+copy.jpg

Thursday 27 June 2013

NDEMBELA SECONDARY YAFUNGWA MKOANI MBEYA



Na Esther Macha, Mbeya
SAKATA la Mgogoro uongozi shule ya sekondari ya Ndembela ambayo inamilikiwa na Kanisa la Wasabato na wananchi wanaoizunguka shule hiyo uliodumu kwa muda mrefu umechukua sura baada ya uongozi wa serikali wilayani Rungwe kupora vifaa vya shule na kutia kufuri majengo ya shule hiyo huku wakiwataka wamilikiwa shule hiyo kukabidhi majengo hayo kwa wananchi.
 
Hata hivyo vifaa ambavyo vimechukuliwa na uongozi wa halmashauri ni pamoja nyaraka, Kompyuta,Samani na vyeti vya Wanafunzi .
 
Akizungumzia tukio hilo Kaimu Mkuu wa Shule hiyo Brown Osward alisema
kuwa siku ya tukio hilo viongozi mbali mbali wa halmashauri walifika shuleni hapo akiwemo Mwanasheria wa halmashauri ,Ofisa Utumishi pamoja na viongozi wengine wa kata na vijiji kuvamia jengo la utawala kuvunja milango na kubeba vifaa vyote vilivyokuwepo katika majengo hayo ya
Utawala.

Aidha Osward alizitaja ofisi ambazo zimevunjwa na vifaa kuchukuliwa ni ofisi ya Mkuu wa shule,uhasibu,taaluma na ofisi inayotunza nyaraka za shule ikiwa ni pamoja na vyeti vya Wanafunzi waliohitimu masomo yao katika shule hiyo.

Akizungumzia tukio Mwenyekjiti wa kijiji cha Ndembela Boaz Mwandambo mvutano wa uongozi wa shule hiyo na wananchi ni muda mrefu kwa kuwa mkataba wa kanisa hilo wa kuendesha shule ulikuwa umemalizika hivyo wananchi walikuwa wanahitaji kurejeshewa majengo yao.

“Hawa Wenzetu walipewa majengo ya shule hiyo mwaka 1982 kama
wadhamini nasiyo kuimiliki moja kwa moja lakini kama Wananchi
tulibaini kuwa wanataka kuimiliki shule hiyo kwa miaka 100 ndipo
Wananchi waliposhituka na kuanza kuidai shule yao kwani hawanufaiki
nayo kutokana na ada kubwa inayotozwa katika shule hiyo na
kusababisha watoto wetu kutembea umbali wa zaidi ya kilometa sita
kufuata elimu ya sekondari”alisema

Mkuu wa Wilaya ya Rungwe Crispin Meela alipohojiwa kuhusiana na tukio
hilo alikiri kuwepo kwa mgogoro huo na uamuzi uliochukuliwa na halmashauri huku akidai kuwa kama serikali la wilaya ya Rungwe imeamua kufanya hivyo ili kurudisha shule zake walizokuwa wamezitoa kwa mashirika ya Dini ambapo uongozi wa shule hiyo ulikataa kurudisha.

“Kauli ya serikali Wilaya ni kwamba kuanzia sasa shule hiyo imerudi
Serikalini hakuna mazungumzo tena kwani hao viongozi wa kanisa
tumekuwa tukiwaita mara kadhaa ili waje tufanye mazungumzo lakini
walikataa na tulipata taarifa za kitelejinsia kuwa Wananchi wanataka
kufanya tukio la hatari ndiyo maana tumeamua kutumia njia hiyo ili
waweze kuondoka na kuiachia shule hiyo”alisema

Awali akitoa msimamo wa kanisa hilo ,Mwenyekiti wa kanisa la Adventista Wasabato nyanda za juu kusini Askofu Joseph Mngwabi alisema kuwa serikali kama inahitaji shule hiyo basi tukae meza moja tuzungumze kwani tumesikitishwa na kitendo cha uporaji wa mali za shule.

Alisema kuwa hawajawahi kugombana na halmashauri ya Wilaya ya Rungwe
bali ni wachochezi wachache ambao ni watu wasiopenda maendeleo kwani
shule hiyo imekuwa ikifanya vizuri kitaalamu kwani katika matokeo ya
kidato cha nne 2012 imekuwa ya kwanza Kiwilaya ya Rungwe.

No comments:

Post a Comment