Bi Faith Wairimu Maina akiwa mahakamani Nairobi Juni 19, 2013. Picha/PAUL WAWERU
Na RICHARD MUNGUTI
Kwa Mukhtasari
Mwanamke
mmoja amekiri kortini Nairobi kwamba alikuwa amepanga kulipa watu
Sh200,000 wamuue mumewe. Amewekwa rumande Langata.
NJAMA ya mwanamke za kumkatizia mumewe maisha ilitubuka na sasa amejipata anakodolewa macho na kifungo cha maisha gerezani.
Faith Wairimu
Maina,40, mkazi wa mtaa wa Zimmermann, Nairobi aliyekuwa na hasira za
mkizi aliapa atamuua mumewe Bw John Muthee Guama “kwa sababu alikuwa na
mpango wa kando.“Mimi sijui
kule anakopeleka pesa zake.Kila siku ni mimi nanunulia watoto chakula na
kugharamia mahitaji ya nyumbani. Pesa anazopata mume wangu ni za kulewa
na kustarehesha wanawake wengine,” Wairimu alimweleza hakimu
mwanadamizi Bi Peter Ndwiga.
Akiendelea na
kujitetea alisema, “ Nimekuwa na taabu chungu nzima. Mimi na watoto
wawili wangu tumetaabika vya kutosha huku mume wangu akiendelea na
maisha ya raha mstarehe.”
Alisema kwamba ni yeye huwalipia watoto karo kwa vile “mumewe amewatupa.”
Ili
kufanikisha njama yake aliwakodi watu watatu wa kumuua mumewe na kuahidi
kuwa angewalipa Sh200,000 bila kujua kwamba walikuwa maafisa watatu wa
polisi.
Waliwasiliana
naye na akakubali kuwalipa malipo ya papo hapo ya Sh40,000 na
makubaliano yakawa walipwe masalio baada ya kufikisha kwake mavazi ya
mumewe yakiwa na damu.
Damu
Polisi hao waliwasiliana na
mumewe mwanamke huyo, Muthee, ambaye ni muuzaji wa macadamia, na
wakachukua mavazi yake na kuyalowesha damu kutoka kwa kichinjio na
kuchanganya na damu ya matumbo.
Ushahidi huo uliwasilishwa kortini.
Kutiwa
nguvuni kwa Wairimu Juni 17 kulimshtua alipogundua wanaume watatu
aliopanga nao kwamba angewalipa Sh200,000 kumuua mumewe ndipo arithi
mali yake “walikuwa maafisa wa polisi kutoka kitengo cha Flying Squad.”
Bw Ndwiga
alifahamishwa Wairimu aliota mpango huo wa kumuua mumewe baada ya
kugundua alikuwa na mpango wa kando na mwanamke mwingine kwa jina Njeri
Wambaa.
Hakimu Mkuu Peter Ndwiga ameamua mwanamke huyo azuiliwe rumande gereza la wanawake la Langata akisubiri kuhukumiwa Juni 28.
No comments:
Post a Comment