Mbunge
wa Arumeru Mashariki Joshua Nassari ameshambuliwa na vijana wa Chama
cha Mapinduzi wakiongozwa na Kiongozi wa Chama cha Mapinduzi, Mkoa wa
Arusha aliyejulikana kwa jina la Kalanga na kulazimika
kulazwa katika hopitali ya Selian Mkoani Arusha katika fujo zilizotokea
katika kituo cha kupigia kura cha Zaburi, kata ya Makuyuni, Wilaya ya
Monduli mkoani Arusha.
Akizungumza
kutoka eneo la tukio, Mratibu wa wanawake wa Chadema Mkoa wa Arusha
Sesilia Ndossi alisema “muda wa saa 5 asubuhi tulienda katika kituo cha
kupiga kura cha Zaburi, kumsindikiza Mbunge wa Arumeru ambaye katika
Uchaguzi huo yeye alikuwa Wakala.
"Lakini
tulipofika hapo tulimkuta raia mmoja mwenye asili ya kisomali akiwaita
watu na kuwaambia pigia CCM, ndipo Nassari akamuuliza kwanini unapiga
kampeni kituoni...
"Huyo Baba alihamaki, akamrukia Nassari wakamchangia na Diwani mmoja aliyeitwa Kalanga, wakamsukuma akaanguka damu ikaanza kumtoka puani...
"Baada ya hapo,tukalazimika kuingilia kati na kuondoka na Nassari akaenda mahali tulipokuwa tunalala akabadili mavazi akaenda kutibiwa Minjingu,
"Hata tulipofika huko waliendelea kutufuata wakaja na gari imejaa vijana wa kimasai wakimtafuta Nassari. Tulivyoona hivyo, tulilazimika kukodi gari ambayo hawaifahamu ndipo tukamwondoa kumpeleka Arusha hospitali ya Selian kwa matibabu zaidi."

Taarifa
zaidi kutoka Makuyuni zinasema walipomkosa Nassari walimpiga dereva
wake Gadi Palangyo na Katibu wa Chadema wa Wilaya ya Monduli, Thomas
Kilongola, hadi walipokuja kuokolewa na Mkuu wa Kituo cha Polisi cha
Makuyuni.
Hadi tunaandika habari hii Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha Liberatus Sabas hakupatikana kuzungumzia suala hili baada ya simu yake kuita bila mafanikio.
Hadi tunaandika habari hii Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha Liberatus Sabas hakupatikana kuzungumzia suala hili baada ya simu yake kuita bila mafanikio.
No comments:
Post a Comment