MATANGAZO

/zest+mkali+3.jpg /TULAMCHA+2+copy.jpg

Thursday, 27 June 2013

HALI YA UTANI YAMSABABISHIA KIFO KIJANA MMOJA MKOANI MBEYA



Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya Barakael Masaki.

Ukiuliza Mbeya kuna nini? Ni dhahili kitu cha kwanza unaambiwa kuwa kuna matukio mengi yanayoambatana na vifo yaani mauaji.
Hivi ndivyo ilivyo hata siku ya leo ambapo mauaji tena yametokea katika wilaya ya Momba mkoani hapa na kisa cha mauaji hayo ni utani baina ya mtu na mtu.


Utani uliosababisha mauti kwa Patrick Yohana (30), ulitokana na marehemu huyu kumtania mwenzake ajulikanaye kwa jina la Livingstone Mulyatete@ Mbasa(42) kuwa pikipiki aliyokuwa amenunua ilikuwa mbovu.
Kauli hiyo ilimkasirisha Mbasa mkazi wa Kijiji cha Mwang’ombe wilayani humo na kuamua kuchomoa kisu kikali, kisha kumchoma Patrick katika mbavu zake upande wa kulia.
Tukio hili la kinyama na kikatili lililotokea jana, katika mazingira ambayo marehemu alifikiri kuwa ni utani wa kawaida wakati mwenzake kachoka na maisha.

Kaimu kamanda wa polisi wa mkoa wa Mbeya kamishna msaidizi wa polisi Barakael Masaki amethibitisha kutokea kwa tukio hili.
Masaki amesema kuwa mtuhumiwa huyo amekamatwa na ameiomba jamii kudhibiti hasira zao ili kuepusha madhara yanayoweza kujitokeza.
Bila shaka hata mtuhumiwa pia anajutia kitendo alichokifanya, baada ya kumwaga damu ya mwenzake wakati walikuwa katika hali ya utani na sasa anaambiwa asaidie polisi wakati hajawahi hata kujifunza mafunzo ya jeshi hilo.

No comments:

Post a Comment