MATANGAZO

/zest+mkali+3.jpg /TULAMCHA+2+copy.jpg

Saturday 8 June 2013

FITINA WALIZOFANYIWA TAIFA STARZ,WATANZANIA WAPAMBANA NA ASKARI

Kocha wa Stars, Kim Poulsen kushoto akipambana na askari wa Uwanja wa Marakech
Na Mahmlud Zubeiry, Marakech, IMEWEKWA JUNI 8, 2013 SAA 8:00 USIKU TIMU ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars usiku huu imekiona cha moto mbele ya askari wa Uwanja wa Marakech, baada ya kufanyiwa vurugu na kuzimiwa taa ishindwe kufanya mazoezi kwenye Uwanja huo siku moja kabla ya mchezo wao na wenyeji wao Morocco kesho, kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Dunia.  Sheria za FIFA zinasema timu mgeni, itapewa fursa ya kufanya mazoezi katika Uwanja utakaotumika kwa mechi dhidi ya wenyeji katika muda ambao mechi itachezwa, lakini leo msafara wa Stars ulipofika Uwanja wa Marakech ulizuiwa kuingia ndani na askari wa uwanjani hapo.  Juhudi za Kocha mkuu wa Stars, Kim Poulsen kuwaelewesha askari wa Uwanja huo sheria ili wairuhusu timu kuingia uwanjani hazikuzaa

No comments:

Post a Comment