Dr. Asha-Rose Migiro |
NAIBU
Katibu Mkuu Mstaafu wa Umnoja wa Mataifa, Dk. Ash-Rose Migiro amesifiwa
kwa umahiri wa wake wa kutoingiza athari za kiingereza katika kiswahili,
anapozungumza au kuhutubia, licha ya kuishi na kufanya kazi nje ya
Tanzania kwa miaka mingi.
Amesifiwa
kwamba amekuwa akizungumza kiswahili fasaha kisichochanganywa na
kiingereza, kwa athari za maneno au utamkaji kwenye mikutano ya hadhara
au katika mazungunzo ya kawaida na watu.
Sifa
hizo zimetolewa leo na Mtaalam wa Kiswahili kutoka Baraza la Kiswahili
la Taifa (BAKITA), Mussa Kaoneka, katika kipindi cha lugha ya Kiswahili,
kilichokuwa kikitangazwa na Kituo cha Radio One kilichopo Mikocheni,
Dar es Salaam.
"Hizi
athari zinatokana na watu wengi kupenda kutukuza mno lugha za wenzetu,
na tatizo limekuwa likidhaniwa kwamba huenda ni kitokana na mtu kuwa
ughaibuni kwa mda mrefu, lakini mbona wapo baadhi ya Watanzania ambao
wamekaa na kufanya kazi kwa muda mrefu nje, lakini wakizungumza
Kiswahili utasuuzika moyo kwa jinsi wanavyokienzi wanapoongea", alisema
Kaoneka na kuongeza;
"Mmoja
wa Watanzania hawa naomba nimtaje, ni Dk. Asha-Rose Migiro aliyekuwa
Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, huyu ukimkuta anazungumza kwenye
mikutano ya hadhara hata kwa kutumia hotuba ambayo hakuiandika, huwezi
kumsikia amechanganya hata neno moja la kiingereza katika mazungmzo yake
au kuzungumza kwa haiba ya kizungu.
Kaoneka
alisema, mbali ya hotuba, hata katika mazungumzo ya kawaida Dk.
Asha-Rose ambaye kwa sasa ni Katibu wa NEC ya CCM, Siasa na Uhusiano wa
Kimataifa, akiamua kuzungumza kiswahili ni kiswahili fasaha kisicho na
mchanganyiko wa neno la Kiinereza hata moja.
Katika
kipindi hicho kilichorushwa kuanzia saa mbili asubuhi, kikiongozwa na
mtangazaji Lugendo Madege, walikuwa wanajadili athari mbaya na nzuri za
lugha nyingine kwenye Kiswahili katika zama hizi za utandawazi.
Walisema,
athari nzuri ni pamoja na Kiswahili kuweza kupata maneno mapya hasa ya
majina ya vitu na teknbolojia ambavyo kabla ya udandawazi havikuwepo
Tanzania na hivyo kulikuwa hakuna majina rasmi ya kuvitaja na athari
mbaya ni baadhi ya watu kuchukua maneno ya Kiingereza na kuyapa tafsiri
ya 'sisisi' ambayo yanakiharibu Kiswahili.
Kaoneka
aliyataja baadhi ya maneno yanayotokana na tafsiri za aina hiyo kuwa ni
'Mwisho wa siku' linalotokana na neno la Kiingereza 'at the end of the
day' ambalo kwa mujibu wa mtaalam huyo tafsiri yake sahihi ni
'hatimaye', na mtu kusema "siku hizi nafanyakazi na Benki, wakati
usahihi ni "nafanyakazi benki".
Alifafanua
kuwa kusema, "nafanyakazi na Benki" ikimaanisha kuajiriwa Benki, siyo
sahihi, kwa kuwa kutamka hivyo kuna maanisha kwamba mhusika na benki
wanafanya kazi pamoja. IMEANDALIWA NA BASHIR NKOROMO
No comments:
Post a Comment