Polisi wa Kutuliza ghasia wakifyatua mabomu ya machozi.(Picha ya Maktaba).
Mahmoud
Ahmad Arusha
Jeshi la
polisi limekipiga marufuku chama cha demokrasia na maendelo(CHADEMA)kufanya
shughuli zozote za kuaga miili ya marehemu kwenye viwanja vya Soweto kwani
zoezi la uchunguzi bado linaendelea kwenye viwanja hivyo huku mabomu
yakirindima uwanjani hapo.
Akizungumza
ofisini kwake kamanda wa polisi mkoani hapa Liberatus Sabas alisema kutokana na
uchunguzi unaoendelea wa tukio la bomu kwenye viwanja hivyo imeonelea kuwa si
busara kuweka mkusanyiko wa watu kwani kutaharibu upelelezi.
Kamanda
Sabas alisema kuwa kwa hiyo jeshi hilo limewataka viongozi wa chama hicho
kuwaeleza wafuasi wao mahali sahihi watakapoweza kufanyia shughuli hiyo lakini
si kwenye viwanja hivyo.
Hali kwenye
viwanja hivyo imekuwa ya pilika pilika tangia juzi kwa wafuasi wa chama hicho
kujikusanya tokea asubuhi hadi jioni kwa madai ya kuomboleza tukio la bomu la
kurushwa kwa mkono lililotokea uwanjani hapo juzi.
Hata hivyo
viongozi wa chama cha demokrasia na maendeleo walikuwa wamukusanyana kwenye
uwanja huo hali iliyoendelea kuleta mvutano kati ya viongozi wa jeshi la polisi na wafuasi hao baada ya kukaidi amri ya jeshi
hilo mabomu yalirindima uwanjani hapo.
Baadhi ya
viongozi wa juu wa chama hicho walikuwepo uwanjani hapo akiwemo mbunge wa jimbo
la ubungo John Mnyika,Ezekia Wenje na wabunge mbali mbali wa chama hicho
walikuwa kwenye kikao cha bunge kinachoendelea hali hiyo imeliweka jiji hili
kusimama shughuli zake kutokana na mabomu hayo.
No comments:
Post a Comment