Wananchi wakitembeza kichapo kwa mbakaji huyo mjini Iringa leo ... |
Mbakaji akivuja damu baada ya kupasuliwa na mawe kichwani |
Mtuhumiwa wa ubakaji akipelekwa polisi leo |
Huyu ndie mtoto aliyebakwa na jemba hilo |
mwananchi mwenye hasira kali akimwadhibu kwa ngumi mtuhumiwa wa ubakaji wa mtoto mjini Iringa mchana huu.
......................................................................................................................................................
WAKATI
mkoa wa Iringa ukiwa ni mkoa wa pili kwa maambukizi ya virusi vya
UKIMWI ukiwa nyuma ya mkoa wa Njombe ambao ndio unaongoza huku vitendo
vya ubakaji na mapenzi yasiyo salama vikitajwa ni sababu ,Jemba mmoja
mkazi wa Mwangata katika Manispaa ya Iringa amenusurika kuuwawa na
wananchi wenye hasira kali baada ya kubambwa akibaka kitoto cha
miaka 10 mchana kweupe.
Mashuhuda wa tukio hilo wameueleza mtandao huu kuwa
tukio hilo limetokea mida ya saa8 mchana baada ya mama mazazi wa
binti huyo kusikia mtoto wake akilia kwa uchungu kuomba msaada zaidi
kwa wananchi baada ya kukamatwa kwa nguvu na kijana huyo mbakaji
Mama
mzazi wa mtoto huyo ambae Jina lake na la mtoto wake kwa sasa
yamehifadhiwa na mtandao huu kutokana na sababu za kimaadili
,alisema kuwa wakati tukio hilo likitokea yeye alikuwa akiendelea
na shughuli zake nyumbani na kusikia sauti ya mtoto wake akilia kwa
uchungu kulalamika kubakwa .
Hata
hivyo alisema baada ya kutoka nje na kuelekea eneo hilo ambalo
sauti ilisikika alishuhudia kijana huyo akiendelea kumbaka mtoto
wake jambo lilopelekea kupiga kelele kuomba msaada kwa wananchi
ili kusaidia kumkamata mtuhumiwa huyo wa ubakaji.
Mwanamke
huyo alisema kuwa jitihada za wananchi wa eneo hilo la Mwangata
kumkamata mtuhumiwa ziliweza kufanikiwa pamoja na mtuhumiwa huyo kutaka
kujaribu kukimbia eneo hilo.
Mmoja
kati ya wananchi walioshiriki kumkamata kijana huyo mbakaji
aliyejitambulisha kwa jina la Samweli kalinga alisema kuwa kijana
huyo amekuwa na tabia ya kuwabaka watoto katika eneo hilo la Mwangata
na mara nyingi watoto wamekuwa wakibakwa ila walikuwa hawajui ni
nani anayeendesha vitendo hivyo vya ubakaji .
Hivyo
alisema kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo wa ubakaji kulepelekea wananchi
wenye hasira kali kuanza kumwadhibu kwa kichapo na hata kutaka
kumchoma moto kabla ya baadhi ya wananchi kutumia busura na kutaka
afikishwe kituo cha polisi.
No comments:
Post a Comment