Hapa
Rehema akiwa wodini katika Hospital ya Rufaa ya mkoa wa Iringa
alipokimbizwa kwa matibabu kutokana na kipigo kikali toka kwa askari
huyo, ambaye ni mume wake.Haya ni baadhi ya majeraha ambayo aliyapata
shingoni kutokana na kukabwa shingo na askari huyo.
Bi Rehema akiwa nyumbani kwa wazazi wake baada ya kukimbia nyumba yake kutokana na kipigo kisichokwisha
Mama mzazi wa Rehema akiwa Monica Shauri
Rehema Shauri Madongo ni mmoja kati ya
mwanamke ambaye amebahatika kuolewa na askari polisi kitendo cha
upelelezi ambaye anaeleza jinsi alivyotendewa vitendo vya ukatili wa
kijinsia kwa kuteswa na kupigwa kikatili na pindi anapofika polisi
hakuna hatua zozote zinazochukuliwa kwa mtuhumiwa huyo ambaye ni askari .
Kwa alisema toka ameolewa kila mara
amekuwa akipokea kipigo na mbaya zaidi kabla ya kupigwa amekuwa
akifungwa mikono kwa pingu zinazotumika kuwafunga watuhumiwa pingu
ambazo mume wake huyo amekuwa akizihifadhi ndani ya nyumba.
" Kweli inasikitisha sana kusimulia
kwani kabla ya kupigwa nimekuwa nikifungwa pingu mikono kama mharifu
sugu na baada ya hapo kipigo kikali kimekuwa kikinikuta ....hadi sasa
nimepigwa zaidi ya mara 20 na polisi nimekwenda kuripoti mara tatu na
Hospital nimelazwa mara moja ila siku nyingine nimekuwa nikiugulia
nyumbani ila nyumbani kwa wazazi nimerudi mara tatu sasa"
Alisema kuwa mbali ya kupigwa na
kuumizwa ila kuna mateso mengine ambayo amekuwa akiyapata kutoka kwa
mwanaume huyo ni siri yake na hayapaswi kuelezwa hapa kutokana na jinsi
ambavyo askari huyo anavyomtenda ukatili wa kinyama. Hata hivyo alisema
kuwa akiwa na mimba ya mwezi mmoja hali ya kipigo ilizidi zaidi na
wakati mwingine alipata kumfunga shingo na kanga kwa kutaka kunyonga
shingo huku akitishi kumuua
Aidha alisema kuwa kila akifika
polisi kufungua kesi hakuna utekelezaji unaofanyika kutokana na polisi
kulindana kwa suala hilo. Pia alisema mbali ya kupigwa akiwa nyumbani
kwake ila bado anapoamua kukimbia nyumba hiyo na kukimbilia kwa wazazi
wake bado askari huyo amekuwa akimfuata na kumpa kipigo mbele ya wazazi
wake, tendo ambalo limempelekea yeye na Mama yake
wamekuwa wakiishi ndani wamejifungia
milango kuogopa askari huyo kuja kuwafanyia ukatili, ikiwa ni pamoja na
kuwaua kwa risasi kama ambavyo amekuwa akiwatisha mara kwa mara.
Bi Shauri alisema mbali ya kuwa yeye
ni mmoja wa wacha Mungu kwa maana na Mlokole mzuri ambae kila wakati
asubuhi lazima aende kusali ila kwa sasa anaogopa kutoka asubuhi kwa
kuhofia kuvamiwa na askari huyo . Hivyo aliomba jeshi la polisi kuweza
kumpa ulinzi yeye na familia yake ama kumkamata mtuhumiwa huyo ambae
inadaiwa kwa sasa yupo katika mji wa Iringa.
No comments:
Post a Comment