Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, imetunga sheria ya kupiga marufuku
ndoa za watu wa jinsia moja.Waziri wa Katiba na Sheria wa Zanzibar,
Bwana Abubakar Khamis Bakar, aliyasema hayo kwenye Kikao cha Baraza la
Wawakilishi Zanzibar wakati akijibu swali la Mwakilishi wa Jimbo la
Wawi, Saleh Nassor Juma kutoka Chama cha Wananchi (CUF).
Waziri Abubakar amesema, ndoa za watu wa jinsia moja ni kinyume na
utamaduni wa Zanzibar na kwamba sheria hiyo imeweka adhabu ya kifungo
cha miaka saba kwa wale wote watakaopatikana na hatia hiyo.
Pia alisema kama ninavyomnukuu: "Sheria hii inahusu makosa mengi
yakiwemo ya ubakaji, zinaa, usagaji na umalaya ambayo yote yana adhabu
ya kifungo cha maisha au miaka isiyopungua 30 gerezani," mwisho wa
kunukuu.

No comments:
Post a Comment