MATANGAZO

/zest+mkali+3.jpg /TULAMCHA+2+copy.jpg

Sunday, 5 May 2013

HATIMAYE SIMBA WAICHAKAZA RUVU, WAKIPANDA MPAKA NAFASI YA TATU

Aliyekuwa bingwa wa ligi kuu ya vodacom Simba sc leo wamefanikiwa kurejea katika nafasi ya 3 baada ya kuwaadhibu goli 3-1 Ruvu shootimg ya Pwani. Mchezo uliochezwa katika uwanja wa Taifa.Katika mchezo huo ulioshuhudiwa watazamaji wachache simba walianza kufunguwa ukurasa wa mabao katika dakika ya 14 kupitia kwa Amri Kiemba kwa shuti kali kutoka nje ya eneo la hatari, baada ya kuwahi mpira uliopokonywa na Felix Sunzu kutoka kwa Nyambiso Athuman.
Simba waliendelea kutengeneza nafasi na kushindwa kuzitumia na hivyo kwa Ruvu shooting walio kuwa wanapeleka mashambulhzi machache langoni mwa simba na kupelekea timu kwenda mapumziko Simba wakiwa mbele kwa goli 1-0.
Kipindi cha pili kilianza kwa simba sc kufanya mabadiliko, ambapo Felixs Sunzu alikwenda bench na nafasi yake kuchukuliwa na Mrisho Ngassa.
Katika dakika ya 51 Abdhamman Mussa aliisawazishia Ruvu shooting na kupelekea ubao wa matokeo kusomeka simba 1 - 1 ruvu shooting.
Wakati mashabiki wakijiandaa kutoka katika dakika ya 86 Christopher Edward aliipatia simba sc goli la pili akimalizia mpira uliotemwa na kipa Benjamini Haule kabla ya Ismail Mkoko kuitimisha ukurasa wa mabao katika dakika ya 88 akiunga krosi ya Kiemba, na kupelekea mchezo kwisha kwa simba kutoka na ushindi wa goli 3-1.
Kwa ushindi huu wa leo unaifanya simba sc kufikisha point 42 wakiwa wa meshuka uwanjani mara 24 wakiwa katika nafasi ya 3, huku Kagera sugar wakishuka nafasi ya 4 wakiwa na pointi 40 wakicheza michezo 24.

No comments:

Post a Comment