

Bayern Munich ndio walikuwa wa
kwanza kuchungulia nyavu za BVB Dortmund kupitia Mchezaji wake
M.Mandzukic katika dakika ya 60 goli lililodumu kwa dakika saba tu na
kupelekea timu ya BVB Dortmund kupata mkwaju wa penati na hatimaye
kurudisha goli kupitia kwa Mchezaji wake I. Gundogan katika dakika ya 67
ambaye alipiga penati hiyo kwa ustadi wa hali ya juu na kupelekea
mlinda mlango wa Bayern Kujaribu kuokoa lakini Bila Mafanikio.
Dakika ya 89 kipindi cha Pili
ikiwa imesalia Dakika Moja Mpira Kumalizika Mchezaji wa Bayern Munich
A.Robben aliipatia timu yake ya bayern goli la pili na la Ushindi Ambalo
limewapa Bayern Ubingwa wa UEFA Champion Kwa Mwaka 2013.
Bayern
Munich wameibuka Vinara kwa kuitungua BVB Dortmund kwa Magoli 2 kwa 1
Katika fainali ya UEFA Champion iliyofanyika katika dimba la Wimbley
lililopo katika Jiji La London huko Uingereza 

No comments:
Post a Comment