
HESHIMA
ya ndoa ni kuishi kwa upendo na uhai wake uwe wa hali ya juu. Ndoa idumu
basi, kifo ndiyo kiwatenganishe kama vitabu vya dini vinavyotufundisha.
Kukua kwa
utandawazi kumeleta taswira mpya katika sura ya wapendanao. Sasa hivi
Mtanzania anaweza kuolewa au kuoa raia wa nchi nyingine na kupitia hapo
tunapata kujua mila na desturi za mataifa mbalimbali duniani.

Mtanzania
anaweza kujua tabia za watu wengine kupitia ndoa mseto iliyofungwa,
hivyo kama Mtanzania ataoa au kuolewa na mtu wa taifa lingine halafu
ndoa yao ikasuasua kutoka na tabia ya mtu husika, hakika hiyo itakuwa ni
aibu kwa mhusika na taifa lake kwa jumla.
Nyumbani
ni nyumbani, kwa kulitambua hilo leo tuitazame heshima ambayo mastaa
wetu walioolewa au kuoa nchi jirani wamejijengea na matukio ya aibu
waliyofanya.


MWISHO MWAMPAMBA
Kwa
upande wake yeye alikutana na Meryl Shikwambane aliyekuwa mshiriki
katika shindano hilo akiiwakilisha nchi ya Namibia. Walianza mapenzi
taratibu na kama utani, vyombo vya habari vikaripoti, mapenzi
yakashamiri kiasi cha kufikia hatua ya kufunga ndoa mwaka 2011.
Watanzania
walitamani kuona mafanikio makubwa juu ya ndoa hiyo ambayo ilipata
matunda baada ya kufanikiwa kupata mtoto mmoja ambaye baba yake (Mwisho)
alimuita Monkey (Nyani).
Baada ya
ndoa hiyo, Mwisho hivi karibuni akiwa Bongo ameripotiwa kuanguka kwenye
dhambi ya usaliti wa ndoa ambapo anatajwa katika skendo ya kutoka na
staa wa muziki na filamu Bongo, Baby Joseph Madaha ‘Baby Madaha’.

Baby
Madaha alipohojiwa kutoka na Mwisho kwa ushahidi wa picha alisema hakuna
cha ajabu kwa sababu walishawahi kuwa wapenzi awali hivyo wamerudiana
(kwa hiyo kurudiana kumo hata kama mmoja ameshaoa?!)

Hiyo ni
aibu yetu, Mtanzania anaonesha picha mbaya kwa wenzetu. Hata kama Meryl
hayupo Bongo, anapoona au kusikia matukio kama hayo kwa mume wake,
anapata picha kwamba Watanzania siyo wastaarabu na si waaminifu.

UWOYA NA NDIKUMANA
Ndoa ya
mwigizaji wa sinema za Kibongo, Irene Pancras Uwoya na msukuma kabumbu
wa Rwanda, Hamad Ndikumana ‘Katauti’ nayo ni aibu nyingine! Bibie
Mtanzania ‘pyuwa’ akakutana na jamaa huyo raia wa Rwanda, wakapendana,
mwaka 2009 wakafunga ndoa katika Kanisa la Mtakatifu Joseph jijini Dar.
Ndoa yao
imekuwa ikisuasua, zaidi chanzo kikitajwa ni bibie huyo mwenye mvuto wa
hali ya juu. Ametajwa kuisaliti ndoa mara kadhaa, likiwemo tukio bichi
la kunaswa na Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ katika hoteli ambako
mpaka sasa haijajulikana waliingia kufanya nini.
Kwa tukio
hilo hakika picha mbaya kwa tasnia pamoja na taifa kwa jumla
imejionesha. Uwoya ameshindwa kuitumikia ndoa yake kwa uadilifu kama
alivyoapa mbele ya padri matokeo yake imekosa uhai na kuwa katika hali
ya kifo. Aibu sana!


MFANO WA KUIGWA
Kama ni
pongezi basi zinapaswa kuelekezwa kwa mshiriki mwingine wa Big Brother
Africa 2009, Mtanzania Elizabeth Gupta ambaye ndani ya mjengo alianzisha
uhusiano wa kimapenzi na mshindi wa shindano hilo kutoka Nigeria,
Kelvin Chuwang.
Baada ya
uhusiano huo waliamua wafunge ndoa mwaka 2010, hadi leo ndoa yao
haijatetereka na ikiwa imezaa matunda ya kumpata mtoto mmoja.
Wawili hao maisha yanaendelea bila kuwa na kwaro zozote.
No comments:
Post a Comment