MTANDAO WA WASANII TANZANIA WAJA NA MBINU MPYA KUWAKWAMUA WENYE VIPAJI.
SHIWATA imeandaa maonesho maalum kila
mwezi ili kutoa nafasi kwa wasanii wa fani ya mbalimbali pamoja na
wanamichezo kuonesha vipaji vyao.
 |
Peter Mwenda
|
Wasanii wengi chipukizi wanakosa mahali
pa kuonesha kazi zao, mara nyingi kazi za wasanii wakubwa ndizo ambazo
hurushwa katika redio na luninga (TV).
SHIWATA imeamua kuandaa maonesho haya kwa malengo makuu yafuatayo
(1) Kukuza vipaji
(2) Kuwapatia soko (underground) mahali ambapo wanaweza kuonesha vipaji vyao na kuwashawishi mapromota mbalimbali kuwaajiri.
(3) Kuelimisha jamii kuhusu matatizo mbalimbali kama maadili na magonjwa kama UKIMWI,malaria.
(4) Kuimarisha umoja kati ya wasanii na wanamichezo
SHIWATA inawataarifu viongozi
mbalimbali na makundi ya sanaa na Michezo pamoja na wasanii binafsi
kutakua na mkutano Siku ya Jumatano Aprili 17 mwaka huu saa 8 mchana
katika ukumbi wa Splendid,Bungoni Ilala kupanga ratiba na kupata taarifa
zaidi.
Onyesho la Kwanza litaoneshwa katika ukumbi wa Star Light Hotel, Mnazi Mmoja Dar es Salaam siku ya Jumamosi Aprili 24.
Michezo itakayoneshwa ni pamoja na
maigizo, sarakasi, ngoma, kwaya, karate, Taekwondo, Taarab, Dansi, Bongo
Flava, Mavazi, Gospal na Kasida, mada kuu katika maonesho hayo ni Amani
na Utulivu.
Hii ni nafasi ya pekee kwa wasanii
chipukizi (underground) kuonesha vipaji vyao.Watengenezaji wa filamu,
mapromota, wamiliki wa bendi, MaDj na wanunuzi wa mbalimbali wa kazi za
sanaa wanaalikwa ili waweze kuona vipaji na kununua kazi za wasanii hao
chipukizi.
Wanafunzi wenye vipaji kutoka shule za msingi, Sekondari na vyuo mbalimbali wanaalikwa kuja kuonesha vipaji vyao.
Mipango iliyofanywa ili maonesho haya yarushwe live kituo kimojawapo cha televisheni.
Kutokuwa na chakula kwa wasanii na zawadi mbalimbali zinazotolewa kwa wasanii watakaofanya vizuri katika kila onesho.
Hii
itakuwa nafasi nzuri kwa wapenzi wa burudani ya sanaa kwani kwa muda
mrefu walikuwa hawajui wapi wanaweza kupata burudani kama hiyo kiingilio
kitakuwa bure.
Wote mnakaribishwa
Peter Mwenda 0715/0752- 222677
Ofisa Habari wa SHIWATA
No comments:
Post a Comment