
Producer Marco Chali kutoka MJ Records. Picha na Mwananchi.
Licha ya kuongezeka kwa studio za uzalishaji wa muziki kona za
vichochoro vingi vya Jiji la Dar es Salaam, yeye ni mmoja kati ya
wazalishaji wachache wenye uwezo na kujiamini kwa kuzalisha muziki wa
kizazi kipya maarufu kama Bongo fleva hapa nchini.
Huyu ni Marco Marthias maarufu kama Mako Chali, mwenyeji wa Mji wa
miamba(Mwanza), aliyeingia studio za MJ Rekod miaka ya 2006. Katika
hesabu za haraka mwenyewe anathibitisha kuandaa zaidi ya kazi 4000 za
wasanii mbalimbali tangu alipoingia studio hizo. Mako aliye katika
studio hizo zilizopo Masaki jijini Dar es Salaam,anapata nafasi ya
kuzungumzia ubora wa msanii, changamoto, udhaifu na kazi wanazozifanya.
Anasema kuwa thamani ya msanii wa bongo na maslahi wanayoyapata ni
vitu viwili tofauti. “Msanii wetu anayefanya vizuri katika muziki huu
anatakiwa kulipwa maslahi yanayoendana na thamani yake, kiwango cha
chini kwa wasanii waliopo katika soko kwa sasa wanatakiwa kupata kati ya
Sh18 na 20 milioni kwa shoo moja,”anasema Mako.
No comments:
Post a Comment