MSANII maarufu wa filamu nchini, Kajala Masanja juzi alimwaga chozi kwa
madai ya kujutia utovu wake wa nidhamu aliokuwa akimwonesha mama yake
mzazi siku zilizopita.
Kajala ametoka kukumbana na kashikashi katika maisha yake hivi karibuni,
baada ya kusota jela takriban mwaka mmoja kutokana na kesi ya
kutakatisha fedha iliyomwandama yeye na mumewe ambaye yuko jela.
Akizungumza katika kipindi cha ‘Take One’ kinachorushwa kila Jumanne na
Clouds Tv, Kajala alisema alipokuwa jela alimkumbuka mama yake kwa mambo
aliyokuwa akimwambia na kuanza kujuta kutokana na mateso aliyokutana
nayo huko.
“Mimi nilianza kumkumbuka sana mama yangu alivyokuwa akiniusia kutulia,
ila mimi natoroka nyumbani nakwenda ninakotaka na kumuacha katika
huzuni, ila nilipokaa jela niliona nini umuhimu wa mama, namuomba
anisamehe sikujua nilitendalo,” alisema Kajala.
Aidha, Kajala alisema katika familia yao, mama yake alikuwa ni mkali
kuzidi baba yake, ambaye kila kitu walichotaka kufanya aliwaruhusu,
ikiwa ni pamoja na kwenda katika majumba ya muziki, lakini mama yao
alikataa na kudai sasa anatambua umuhimu wake.
Aliwashukuru wote ambao walikuwa naye bega kwa bega hadi kufanikisha kutoka jela, hukushukrani
za pekee akizimwaga kwa msanii mwenzake Wema Sepetu ambaye alimnusuru
kufungwa jela miaka saba kwa kumlipia faini ya sh milioni 13

No comments:
Post a Comment