BAADA ya
zile dawa za Kichina za kuongeza makalio, ‘hips’ na matiti zilizotikisa
Bongo na kubainika kubeba madhara makubwa kama vile ‘kalio’ moja kuwa
kubwa kuliko lingine, kujazia zaidi chini kuliko juu na mwili kufa
ganzi, zilikosa soko, lakini sasa zimeibuka nyingine za kienyeji
Uchunguzi
uliofanywa na blog kupitia kwa wataalam mbalimbali wa
tiba za asili TANZANIA , ulibaini kuwa dawa hizo zimejaa tele kwa
waganga wa kienyeji.
Ilifahamika pia kuwa hivi sasa dawa hizo zinachangamkiwa na wanawake
ile mbaya wakiamini kwamba hazina madhara kama zile za Kichina.
NI MCHANGANYIKO WA MITI 60
Mmoja wa wataalam hao aliyezungumza na blog hii alisema
kuwa, dawa hiyo ni mjumuisho au mchanganyiko wa miti zaidi ya 60
inayopatikana kwenye misitu mikubwa hasa mikoani.
JINA LAKE
jina la dawa hiyo, mtaalam huyo alisisitiza:“Nimeshakuambia
ni mchanganyiko wa miti zaidi ya 60, haina jina isipokuwa mteja akifika
anatakiwa aseme kama anataka mzigo wa saizi gani.”
Mtaalam
huyo alikwenda mbele zaidi na kuweka kweupe kuwa dawa hiyo ni kiboko ya
Mchina kwani dozi na bei yake hutegemea aina ya kalio analolitaka mteja
husika.
“Ukitaka dogo, la kati au kubwa, kila moja lina dozi na bei yake hivyo inategemea mteja amechagua la aina gani,” alisema mtaalam huyo. WATAALAM WA TIBA ASILIA WANASEMAJE?
waandishi wa audifacejackson blog waliendelea kufanya mahojiano na
wataalam mbalimbali wa tiba za asili ambapo walikuwa na haya ya kusema:
MJUKUU WA BABU
Mganga maarufu kwa jina la Mjukuu wa Babu anayepatikana Mwananyamala jijini Dar es Salaam alifunguka:
“Nakwambia hii dawa ni kiboko ya zile za Kichina. Ni dawa nzuri na
kusema kweli watumiaji ni wengi. Ni mchanganyiko wa miti zaidi ya
sitini ambao huwa unatoa aina moja ya dawa.

No comments:
Post a Comment