Dah naskia jana
kwenya interview yake na TBC alimchana Ruge live, tunajaribu kuifuatilai
interview hiyo na tutawaletea hapa live kila kitu alicho kiongela super
star huyo. Stay tuned!
Kwa wale ambao hamuelewi mkasa huu pitia hii habari hapa chini ambayo
meneja wake Gardner Habash aliamua kufunguka na kuzungumzia tweet za
mkewe huyo.
KUTOKANA na msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini Judith Wambura 'Lady
JayDee' kuonekana kutuma 'Tweets' zilizobeba mafumbo huku akitoa mazito
ya moyoni juu ya mtu anayemvurugia mipango yake ya kimuziki hakuweza
kumtaja jina mume wake Gadna Habash afunguka juu ya 'Tweets' hizo
Akizungumza jijini Dar es Salaam hili hivi karibuni Gadna alisema kuwa
'tweets' alizoziweka msanii huyo zinalenga kufikisha ujumbe alioukusudia
hususani kwa baadhi ya watu wanaomuwekea mipango mibaya ya kuharibu
kazi zake za kimuziki
Alisema kuwa wapo baadhi ya washika dau wanaojikita katika maswala ya
muziki kwa ajili ya maslahi yao binafsi huku wakimnyonya mwanamuziki
bila ya kujali jasho lake na nguvu yake kwa kazi anayoifanya
Kutokana na hali ya kunyonywa wasanii na washika dau hao alisema msanii
atakapopata akili na kuwa na uwezo wa kugundua kuwa ananyonya na hawezi
kufika mbali hali inabadilika kwa kuanza kukandamizwa na kuwekewa
vikwazo katika kazi zao
"Baadhi ya washika dau wanawaogopa wasanii wakubwa kwa kuwa tishio
katika biashara zao hivyo hata wasanii wachanga pia wananyimwa nafasi ya
kukua kisanii kwa kuhofia kuja kuwageuka baadaye pindi watakapopata
nafasi ya kufanya hilo" alisema Gadna
Aliongezea kuwa mfumo wa muziki hauko sawa na upo kwa lengo la kumnyonya
msanii hali ambayo inazidi kudidimiza wasanii na muziki wa nchi hii
hali inayosababisha muziki unakuwa kwa kusikilizwa redioni na si kwa
kukuwa kwa kipato kwa wasanii
Alisema kuna hujuma zinazoendelea kwenye soko la muziki zenye lengo la
kumnyonya mwanamuziki na kumpa utajili mdau wa muziki sababu hiyo
inapelekeea wanamuziki wa nchi yetu kutoendelea katika soko la muziki
Lady JayDee hivi karibuni amekuwa akitumia mtandao wa Twitter kwa ajili
ya kutuma 'tweets' zenye ujumbe kwa mtu aliyemkusudia ingawa
hazikuonyesha wazi wala kutaja jina la muhusaka
Hizi hapa chini ni baadhi ya 'tweets' zilizotumwa na msanii huyo hapo nyuma
Lady JayDee ?@JideJaydee
Hata nyimbo zisipopigwa now mi sio underground, won't complain. Nani asiemjua JayDEe? Am not crazy
Lady JayDee ?@JideJaydee
Basi mjue kuwa tatizo langu sio nyimbo kutopigwa redioni. Its more than that. U dig??
Lady JayDee ?@JideJaydee
Now nategemea nguvu ya uma #diehardfans
Lady JayDee ?@JideJaydee
Na tweet
hivi sbb sikuwahi kulalamika nikaamua kufanya kazi. Lakini kazi
inapowekewa uzito wa jiwe isipenye. That's another case...
|
No comments:
Post a Comment