MSANII wa muziki wa Kizazi Kipya na Filamu Bongo, Zuwena Mohamed
‘Shilole’,jana alianika wazi tabia yake ya uchunaji mabuzi alipokuwa
kwenye moja ya mahojiano na watangazaji wa Kipindi cha Leo tena cha
Clouds FM, baada ya kuulizwa swali liloendana na jina la kibaochake
kipya ambacho jana ndiyo ilikuwa siku rasmi akikiachia hewna kupitia
stesheni za radio hiyo,baada ya kuachia ngoma yake mpya inayokwenda kwa
jina la NACHUNA BUZI,
mmoja ya watangazaji wa kipindi hicho alimuuliza ni
kitugani kilichompelekea hadi kutunga wimbo wa namna hiyo na kuupa jina
hilo,Shilole katika majibu yake alisema kuwa ameamua kukipa jina hilo
kufuatia historia mbalimbali za maisha yake,hususani wimbo wake uliopita
ambao aliupa jina la
Nakomaa na jiji la Dar,sasa kudhihirisha kauli
hiyo ameamua kuchuna mabuzi ili aweze kupata mkwanja wakutosha
kulihimili jiji la Dar es Salaam na Igunga abaki kwenda kusalimia ndugu
na jamaa tu.Baada ya manene hayo Shilole pia aliandika ujumbe huu kwenye
ukurasa wake wa Instagram:-
shilolekiunoASANTENI MASHABIKI WANGU WOTE KWA KUIPOKEA VEMA NYIMBO YANGU MPYA#CHUNABUZI# MUNGU AWABARIK# AMEEN
No comments:
Post a Comment