Mwanafunzi akiwa kitandani tayari kwa kutolewa mimba
MUUGUZI wa
kike, Violet Shoo, mkazi wa jijini Dar ametiwa mbaroni na Jeshi la
Polisi Kituo cha Buguruni, Ilala baada ya kunaswa katika jaribio la
kutaka kumchoropoa ujauzito msichana mmoja aliyepandikizwa kama
mwanafunzi kwa mtego makini ulioratibiwa na Oparesheni Fichua Maovu
‘OFM’
Tukio hilo lilitokea Jumamosi ya wiki iliyopita, saa 11 jioni kwenye zahanati iliyopo Tabata Matumbi, jijini Dar es Salaam.
Nesi akidhibitiwa na polisi...
Muuguzi huyo
alikutwa ndani ya zahanati hiyo akiwa na zana mbalimbali zinazodaiwa ni
za kutolea mimba huku msichana huyo akiwa juu ya kitanda, tayari kwa
kufanyiwa zoezi hilo haramu.
Awali,
Ijumaa ya Mei 23, mwaka huu baadhi ya wakazi wa eneo hilo walitutumia
ujumbe wakimlalamikia muuguzi huyo kwamba amekubuhu katika matukio ya
utoaji mimba hivyo wakaomba ikiwezekana OFM imuandalie mtego wa kumnasa
ili kukomesha kitendo hicho.
“…huyu nesi
amekuwa akiwatoa watoto wetu mimba, kwa siku anaweza kutoa hadi nne,
sisi wazazi tumechoshwa, tunaomba mje. Anaitwa Violet…” ilisomeka sehemu
ya meseji hiyo huku ikielekeza zahanati anapopatikana.
Nesi akiwa chini ya ulinzi....
Baada ya
malalamiko hayo, kikosi cha upelelezi cha OFM chenye wasichana wawili
kilikwenda kwenye zahanati hiyo na kukutana uso kwa uso na muuguzi huyo
ambapo msichana mmoja aliomba kutolewa mimba na nesi huyo ambapo
aliambiwa ni shilingi 50,000.
Kikosi kiliondoka kwa kumwambia muuguzi huyo kwamba wanafuata fedha mahali na wangerejea jioni wakiwa na pesa mkononi.
Timu ya
waandishi wetu wa habari pamoja na Jeshi la Polisi waliweka mtego baada
ya wakazi wa maeneo iliyopo zahanati hiyo kulalamika juu ya kukithiri
vitendo vya utoaji mimba vinavyofanywa kwa muda mrefu na muuguzi huyo.
Wakazi wa
maeneo hayo ambao hawakupenda majina yao yaandikwe , walidai kwa njia ya
ujumbe mfupi wa maandishi na kupiga simu katika chumba cha habari kuwa
idadi kubwa ya wanawake wanatolewa mimba kwa siku katika zahanati hiyo
bubu ambayo haina jina wala hadhi ya kutoa huduma.
Baada ya hapo, waandishi hao wa kike walirejea ofisini na kutoa taarifa kwa mabosi wao ambapo timu kamili ilipangwa.
Mkuu wa timu
hiyo alianzia Kituo cha Polisi Buguruni ambapo alitoa taarifa kuhusu
malalamiko ya wakazi wa eneo hilo na jinsi muuguzi huyo alivyofikia
hatua ya kutaka alipwe elfu hamsini ili kukamilisha zoezi.
Afande mkuu akatoa maagizo kwa watu wa chini yake watatu, akiwemo askari wa kike mmoja kwa ajili ya kwenda kumnasa nesi huyo.
Msichana
aliyepandikizwa kutolewa mimba akiwa na mwenzake walitangulia kufika
kwenye zahanati hiyo lakini hawakumkuta muuguzi huyo.
Mfanyakazi
mmoja wa zahanati hiyo alimweleza ‘mtolewa mimba’ kwamba nesi huyo
alikwenda kusuka na tayari ameshawasiliana naye hivyo wasubiri.
Saa kumi
na nusu, muuguzi huyo aliwasili kwa ajili ya kazi hiyo huku mawasiliano
yakifanyika kati ya mtolewa mimba na waandishi waliokuwa jirani na eneo
la tukio.
Ndani ya
dakika kumi, waandishi na polisi waliitwa eneo la tukio wakijulishwa
kwamba ‘mjamzito’ huyo ameshavua nguo tayari kwa kazi ya kuchoropolewa
mimba.
Kikosi
kazi kilivamia zahanati hiyo ambapo walikuta zoezi linaendelea. Polisi
wenye ujuzi wa kazi za kunasa matukio walimtia mbaroni muuguzi huyo
akiwa na zana za shughuli huku wakimwambia kosa lake.
Vifaa vilivyotumika....
Wakati huo, mjamzito alikuwa yupo kitandani katika maandalizi ya kutolewa mimba.
Wananchi
waliokuwepo eneo la tukio wakati mtanange ukiendelea, walionekana
kufurahishwa na kitendo cha kukamatwa kwa muuguzi huyo huku wakidai
walikuwa wamechoka naye kutokana na vitendo vyake vya kutoa mimba hadi
kwa wanafunzi.
“Tumekuwa
tukijitahidi kutoa taarifa katika vyombo vya dola ikiwemo ofisi ya
mwenyekiti wa serikali ya mtaa wetu lakini hakuna hatua zozote
zilizokuwa zikichukuliwa, ndiyo maana tukaamua kuwasiliana na nyie
waandishi wa habari ili mtusaidie,’’ alisema mkazi mmoja bila kutaja jina lake.
Muuguzi huyo alipoulizwa kwa nini amekuwa akijihusisha na vitendo hivyo, alikaa kimya.
Mjumbe wa
Nyumba Kumi, Shina Namba 26, Tawi la Mandela, Rogasian Chadima alikuwepo
katika eneo la tukio baada ya kufuatwa na polisi, naye aliahidi
kufuatilia suala hilo akisema kwanza hakujua kama kuna zahanati katika
eneo lake.
No comments:
Post a Comment