Kesi ya wanaume kupungukiwa nguvu za kiume zimezidi kushika kasi, kiasi cha kufanya dawa za kuongeza nguvu hizo kuwa maarufu na zenye mahitaji makubwa katika jamii.
Waganga
wa kienyeji wamekuwa wakitumia dawa hizo kama tiba ya msingi ya
kuwavutia wateja kwenye biashara zao. Hii inaonesha kuwa tatizo hili ni
kubwa miongoni mwa wanaume wengi katika jamii yetu.
Hata
hivyo, utafiti unaonesha kwamba wengi kati ya wanaume waliowahi kutumia
dawa za asili na zile za hospitali kuondokana na tatizo la upungufu wa
nguvu za kiume hawakufanikiwa kupata tiba ya kudumu, matokeo yake
wamegeuzwa kuwa watumwa wa kila wanapotaka kushiriki tendo lazima wabwie
‘kolezo’ la kuwasaidia kuamsha hisia zao.
Kwa
wanaume, ukosefu wa nguvu ni jambo linalouma na kuondoa kabisa ujasiri.
Wengi kati yao wako tayari kutumia pesa na uwezo wao wote kuhakikisha
kuwa heshima ya tendo la ndoa ikuwa katika miliki yao daima.
Lakini,
watafiti wa masuala ya mapenzi nikiwemo mimi, tumegundua kuwa wengi
kati ya hao wanaolalamika kupungukiwa nguvu za kiume, hawafahamu chanzo
cha matatizo na namna wanavyoweza kuepukana na kasoro hizo.
Ushahidi
uliopatikana kwa waathirika wa tatizo hili, unaonesha kuwa wanaume
wanapokabili upungufu wa nguvu za kiume huishia kujuta na kujilaumu
wenyewe bila kutazama upande wa pili wa washirika wao, namaanisha
wanawake.
Zipo
kesi za wanaume kujiua au kujinyofoa sehemu zao za siri kwa sababu ya
kushindwa katika tendo la ndoa. Hali hii inatoa picha kwamba wanaume
wengi hujitwika mzigo wa lawama wenyewe.
Dokta
Bianca P. Acevedo kutoka Chuo Kikuu cha California, Santa Barbara
anasema, wanawake huchangia kwa kiasi kikubwa tatizo la upungufu wa
nguvu za kiume, jambo ambalo nami nalithibitisha kwa ushahidi wa
kitaalamu ufuatao:
1: KAULI
Miongoni
mwa mambo ambayo mwanaume hataki kuyasikia yakitoka kwenye kinywa cha
mwanamke ni kuambiwa HAWEZI TENDO LA NDOA. Mwanamke akimwambia mwanaume
wakati au baada ya tendo kuwa hawezi, atakuwa amemsababishia tatizo
kubwa la kisaikolojia ambalo litampelekea kupotea nguvu za kiume
taratibu.
Msaada
unaohitajika kwa mwanamke anayekutana na mwanaume dhaifu kwenye tendo
si kumwambia hawezi, bali ni kumtia moyo na kumsaidia kuweza. Wanawake
wamewasababishia waume zao upungufu wa nguvu za kiume kwa kuwaambia
maneno kama haya: “Yaani siku hizi sijui umekuwaje, yaani huwezi kazi
kabisa!”
2 : UJUZI
Wanawake
wengi hasa waliopo kwenye ndoa, wanapuuza ujuzi kwenye tendo la ndoa.
Hawajishughulishi kumsaidia mwanaume ‘kuwika’, si wabunifu na watundu,
jambo hili humfanya mwanaume kushiriki tendo kwa kutegemea kupanda kwa
hisia zake mwenyewe, hivyo anapokuwa amechoka au ana mawazo, hawezi
kusisimka kwa vile hapati ushirikiano toka kwa mwenzake.
Pamoja
na wengi kutokuwa wajuzi, lakini wapo wengine ambao ni watundu mno
kwenye sita kwa sita kiasi cha kumfanya mwanaume ajione kama mgeni wa
mchezo huo.
Kimtazamo,
wanaume hupenda sana ushindi wakati wa ‘kazi’, lakini pale wanapogeuzwa
‘chekechea’ hupunguza uwezo wa kujiamini na kuruhusu hofu kuongezeka
mawazoni mwao, hivyo kuwasababishia tatizo la upungufu wa nguvu za
kiume.
Inashauriwa
kwamba, mwanamke anapokuwa na uelewa mkubwa wa masuala ya mapenzi hasa
wakati wa tendo, asioneshe kiwango kikubwa kwa haraka bali amchukulie
mwenzake kama mwanafunzi, asiwe na maneno kama: “Leo nakuja kukupa vitu
adimu kuliko vya juzi, hakuna kulala kasi mtindo mmoja.” Kauli hizi
huwaogopesha wanaume na kuwafanya wapungukiwe na nguvu.
USAFI
Mwanamke
anapokuwa si msafi, huweza kumsababishia mwanaume matatizo ya upungufu
wa nguvu za kiume. Sote tunafahamu umuhimu wa usafi wa mwili na kero za
uchafu wakati wa tendo, hivyo ni wazi kuwa mwanamke akiwa mchafu
atamfanya mwanaume apoteze msisimko na uwezo wa tendo la ndoa. Unadhifu
wa mavazi na mwili ni muhimu sana katika mapenzi.
GUBU
Jambo
lingine linaloweza kumsababishia mwanaume upungufu wa nguvu za kiume ni
gubu au karaha za maneno ya uchokozi yasiyokuwa na kichwa wala miguu.
Uchokonozi wa mambo, ugomvi, usaliti na hali ya kutokuwa na staha ni
mambo yanayosababisha tatizo la upungufu wa nguvu za kiume.
Mwanamke
anapokuwa mwingi wa maneno ya kashfa, dharau na matusi huweza kumfanya
mume amchukie na kutopenda kushiriki naye tendo. Uchunguzi unaonesha
kwamba wanawake walioolewa wenye tabia hii, huwafanya waume zao wawe na
msisimko wa kimapenzi kwa wanawake wa nje kuliko wake zao hao.
USALITI
Tabia
ya usaliti kwa mwanamke ni chanzo kingine cha mwanaume kupata tatizo la
upungufu wa nguvu za kiume. Mwanaume anapoona, kuhisi au kubaini kuwa
anasalitiwa, huumia sana moyoni, maumivu ambayo hatimaye humfanya
muhusika kuwa na mawazo mengi ambayo humuondolea hamu ya tendo.
No comments:
Post a Comment