MATANGAZO

/zest+mkali+3.jpg /TULAMCHA+2+copy.jpg

Tuesday, 31 December 2013

HII NDO NYUMBA ALIYOZALIWA MSANII LADY JAY DEE TIZAMA PICHA

BALAAA UMASIKINI WASABABISHA MUME KUUZA KABURI LA MKEWE NA KUZUA VARANGATI...............

 
Hii ndiyo kali ya kufungia mwaka katika zote zilizotokea mwaka 2013! Mwanaume aliyetajwa kwa jina moja la Abrahaman, mkazi wa Kimara-Kilungule, Dar, anadaiwa kuuza kiwanja ambacho ndani yake kuna kaburi marehemu mkewe, Aisha Abdul aliyefariki Julai 21, 2004.
MALALAMIKO MEZANI
Wakizungumza na Uwazi kwa nyakati tofauti, watoto wa marehemu ambao wanapingana na tukio hilo la baba yao kuuza eneo hilo ambalo ni mali ya marehemu mama yao, walidai kuwa wamefedheshwa na kitendo hicho.
 

“Kiukweli alichokifanya baba siyo sawa. Haiwezekani auze eneo ambalo lipo kaburi la mama yetu. Mbaya zaidi hadi sisi watoto wa kutuzaa yeye mwenyewe anatutishia maisha.
“Anatufukuza katika nyumba kisa kwa nini tunamuhoji tabia yake ya kuuza maeneo aliyoyaacha marehemu mama,” alisema Tunu ambaye ndiyo msimamizi mkuu wa mirathi. 
Watoto hao walidai kuwa baba yao anauza mali huku akijua kabisa mama yao aliacha wosia juu ya nani mrithi wa mali hizo (kopi ya wosia tunayo).
“Hatujui nini kimemkumba baba maana amekuwa mkatili asiyekuwa na huruma ya aina yoyote kwetu hadi na kwa majirani,” walisema watoto hao. 
USHUHUDA
Gazeti hili lilifika eneo la tukio na kulishuhudia kaburi hilo huku watoto hao wakipiga nalo picha kwa woga wasikute na aliyeuziwa.
Pia majirani walithibisha ukali wa baba huyo katika siku za hivi karibuni.
 

Katika hali ya kushangaza, wakati watoto hao wakitoa malalamiko hayo walianza kugawanyika kifamilia ambapo mmoja wa mwisho wa kiume alikuwa upande wa baba akiunga mkoni kile alichokifanya mzazi wake huyo.
Baada ya kusikia malalamiko hayo na kuoneshwa vielelezo, ilibidi kumtafuta mume huyo wa marehemu ili kuthibitisha madai hayo. 
Alipopatikana alipelekewa tuhuma zake juu ya sakata ambapo bila hata kusikia kwa makini alichokuwa akielezwa alianza kutukana huku akilichimba mkwara Uwazi kufuatilia habari zake.
“Endeleeni kunifuatilia lakini mtakachokiona nisilaumiwe,” alisema baba huyo aliyeonekana kuwa na umri mkubwa. Katika hitimisho, watoto hao walishauriwa kwenda kwenye vyombo au mamlaka za kisheria ili kupata haki zao.

WANUSURIKA KIFO BAADA YA DALADALA KUACHA NJIA GONGO LA MBOTO

Gari hilo pichani likiwa limetumbukia kwenye mitaro ya pembeni mwa barabara eneo la Gongo la Mboto na askari wa usalama barabarani wakijitahidi kuyaondoa magari yaliyogogwa na gari hilo, huku baadhi ya wananchi wakishuhudia.
Gari hilo pichani likiwa limetumbukia kwenye mitaro ya pembeni mwa barabara eneo la Gongo la Mboto na askari wa usalama barabarani wakijitahidi kuyaondoa magari yaliyogogwa na gari hilo, huku baadhi ya wananchi wakishuhudia.
Gari hilo pichani likiwa limetumbukia kwenye mitaro ya pembeni mwa barabara eneo la Gongo la Mboto na askari wa usalama barabarani wakijitahidi kuyaondoa magari yaliyogogwa na gari hilo, huku baadhi ya wananchi wakishuhudia.
Gari hilo pichani likiwa limetumbukia kwenye mitaro ya pembeni mwa barabara eneo la Gongo la Mboto na askari wa usalama barabarani wakijitahidi kuyaondoa magari yaliyogogwa na gari hilo, huku baadhi ya wananchi wakishuhudia.
ABIRIA wa daladala moja namba T608 BKP aina ya Toyota Hiace eneo la Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam leo wamenusurika kifo baada ya gari hiyo iliyokuwa ikielekea Moshi-Baa kupata ajali ikiwa inawakimbia wafanyakazi wa SUMATRA, ajali hiyo imetokea leo majira ya jioni baada wa dereva wa daladala hiyo kuona gari la Sumatra na kuanza kutimua mbio bila kujali usalama wa abiria.
Dereva huyo aliyekuwa anatumia barabara za pembezoni mwa barabara kuu alianza kuendesha gari hilo kwa kasi na baada ya askari kumuona walimfuata na kumzuia ili wamuhoji baada ya kuzuiwa kwa mbele gafla aliondoa gari kwa kasi na kuingia uchochoro mwingine kisha kutaka kuingia barabara kubwa kwa kasi ndipo alipogogana na gari lingine dogo lililokuwa likipita.
Kama vile mchezo wa kuigiza wa mbio za magari dereva huyo aliwasha tena gari hilo likiwa tayari limeumia na kutaka kukimbia kwa kasi ndipo lilipomshinda na hatimaye kuingia mtaroni na kukwama. Ghafla dereva huyo alishuka kwenye gari na kuanza kutimka lakini askari na baadhi ya wananchi walimtia mikononi baada ya hatua chache ndipo wananchi wenye hasira wakaanza kumpiga hadi walipo zibitiwa na askari waliofika eneo la tukio hilo muda mfupi.
Abiria walianza kujinusuru kwa kutoka ndani ya gari hilo wakikimbia huku wengine wakitokea madirishani. Hata hivyo mmoja wa abiria alizimia kutokana na tukio hilo hivyo kukimbizwa hospitalini kwa msaada zaidi. Baadhi ya mashuhuda waliozungumza na mtandao huu walisema dereva huyo alikuwa akiwakimbia Sumatra kwani daladala hiyo ilikuwa ni bubu hivyo alihofia kukamatwa ndipo alipoanza kutimua mbio hovyo. Hata hivyo hakuna abiria aliye jeruhiwa kwa ajali zote mbili zilizotokea wakati gari hilo likitimua mbio.Credit: The Habari.com

MWANAMKE AUWAWA KIKATIRI KWA KUCHOMA NA VISU MJINI IRINGA SOMA ZAIDI


 

Waombolezaji  wakiwa  katika msiba  huo  eneo la Mtwivila 

 

Mume wa marehemu Bw Hamza Kidava na mtoto wake  wakitoa heshima  za mwisho  kabla ya mazishi 

 

mwili  wa marehemu Doris Lyandala

 

Kaburi la marehemu Doris

 

Aliyekuwa  mume wa marehemu Doris Lyandala Bw Hamza Kidava kushoto akiwa na rafiki  zake nyumbani kwao Mtwivila leo

 

Bw Hamza Kidava  akiwa katika majonzi mazito

 

Bw Hamza Kidava  akionyesha  eneo  ambalo mke  wake kipenzi alipouwawa kwa  kuchomwa visu na mtu anayesadikika kuwa ni kichaa

 

Bw Hamaza kushoto akimwonyesha mwandishi wa mtandao huu mzee wa matukio  daima hayupo pichani na Bw Brown eneo ambalo mke  wake aliuwawa


Dereva  Taxi  aliyekuwa akimwendesha  Mzee wa matukio  daima  Bw Brown akiwa nje ya nyumba aliyekuwa akiishi mtuhumiwa wa mauwaji  ya Bi Doris Lyandala
HAKUNA Kati  yetu  ajuaye siku yake na  kufa na kifo  chake kitakuwaje na kama ungelijua lijalo mbele  yako hakuna ambaye angejaribu kutoka ndani ya nyumba yake kwenda  kukutwa na mauti.


Ni kauli  za  majirani  na marafiki wa karibu wa mrembo Doris  Lyandala  ambae kwa sasa kwa wakazi wa mji wa Iringa jina lake  ndilo limeendelea kutesa mawazo ya  wengi.


Doris ambae enzi za uhai  wake alipata  kuwa mmiliki wa Saloon yake ya kutengeneza  nywele  warembo wenzake na alipata kuwa mcheshi asiyependa makuu tulitamani tungekula na  kusherekea nae pamoja  Krismas  ambapo ilibaki siku moja pekee kula Krismas na rafiki ,familia yake na  zilibaki  siku takribani  7  kuuaga mwaka 2013 na kuukaribisha mwaka 2014 ila yote hayakuwezekana na badala  yake rafiki na ndugu walijikuta  katika simanzi ya kifo chake .


Mmoja kati ya marafiki zake wa karibu  Salima Alli alisema  kuwa alikuwa ni mteja  wake mkubwa katika  saloon na kabla ya  kukutwa na umauti  siku moja kabla alipata  kumseti nywele  zake.


Bw Hamaza Kidava  ndie mume wa marehemu  huyo anasema kuwa alipata  taarifa  kutoka kwa majirani  kuwa kipenzi chake mke wa mtoto mmoja amepatwa na tatizo na amekimbizwa katika  Hospital ya Rufaa ya mkoa wa Iringa.


Alisema kuwa baada ya  kufika Hospital hapo hakuamini  kuona mke aliyempenda kuliko akitokwa na damu huku akieleza kwa  shida  kilichomkuta .


Akizungumza kwa uchungu mwigi huku akilengwa na machozi Hamza ambae ni mmoja  kati ya vijana watanashati na wenye ajira zao akiwa katika  sekta ya kutengeneza simu alisema  kuwa alichoelezwa  kuwa amechomwa visu na kichaa.


"Ina  niuma  sana  kumpoteza mke  wangu na ina niuma sana kuona  leo  nimebaki mpweke nikilea mtoto mmoja ambae nimezaa nae mke  wangu Doris ....kaka nashukuru kwa  kuja  kunifariji na  nawashukuru wote  walioshiriki kuuguza hadi mazishi  yake "alisema Hamaza  kumaliza kwa kusema twende nikakuonyeshe alipokutwa na mkasa huo  wakati akitoka dukani kutafuta mahitaji.


Ndudu wa karibu na mtuhumiwa wa mauaji  hayo ambae hakupenda  jina lake  kuandikwa hapa kwa kuwa si msemaji wa familia alisema  kuwa  mtuhumiwa  huyo wa mauwaji Bw Zakayo Lwambano (26) ni mkazi wa Mtwivila na alikuwa akiishi  mtaa mmoja na marehemu Doris .


Alisema  kuwa kijana  huyo Zakayo alianza kuugua ugonjwa  huo toka mwaka 2010 ambapo ndugu  walimpeleka Hospital ya vichaa Milembe Dodoma na kurejea akiwa mzima wa afya.


Hata  hivyo alisema  baada ya  kurejea  alikuwa ni mtu aliyetulia na kujipatia  kipato chake cha kila siku kwa  kufanya kazi ndogo ndogo za kusomba mchanga na nyingine kwa  wananchi wa eneo hilo .


Ndugu  huyo alisema wazazi wa mtuhumiwa huyo kwa  sasa  walisha fariki dunia na alikuwa akiishi peke yake katika getho ( nyumba yake ya chumba kimoja )  aliyojenga  mwenyewe
Alisema  kuwa  siku ya tukio Desemba 24 kabla ya kumshambulia Mrembo  huyo alianza kumchoma  kisu ndugu  yake James Moyo (28) ambae  alifika nyumbani hapo kwa  ajili ya kula sikukuu  akitokea Makambako Njombe.


Alisema kijana  huyo aliyejeruhiwa alikuwa akiishi nyumba nyingine tofauti na getho la mtuhumiwa na alichomwa  visu viwili kwapani na kukimbizwa Hospital ya rufaa ya mkoa wa Iringa na kwa sasa ameruhusiwa na kurejea Makambako kwao.


Pia  alisema mtuhumiwa  huyo baada ya mauwaji alijipeleka mwenyewe polisi na kutaka awekwe ndani kwa madai ameua
Jeshi  la  polisi  mkoa wa Iringa  limethibitisha  kutokea kwa mauwaji hayo na kuwa  mtuhumiwa huyo hadi sasa anashikiliwa na polisi .


Kamanda wa  polisi wa mkoa wa Iringa Ramadhan Mungi  alisema  kuwa mwanamke  huyo alichomwa visu sehemu mbali mbali ya mwili  wake na baada ya  kukimbizwa  Hospital akiendelea na matibabu alifariki dunia.


Alisema kuwa   mtuhumiwa   huyo amenashikiliwa kama  watuhumiwa wengine na kuwa mwenye mamlaka ya kumfunga ama kutomfunga ni mahakama na  wao kama polisi hawajui kama ni kichaa wanajua kama mtuhumiwa wa mauwaji.


Mtandao  huu na  wadau wake  unatoa pore  nyingi kwa familia ya Kidava na Lyandala pamoja na ndugu na jamaa wote ambao  wameondokewa na mpendwa  wao ambae sote  tulimpenda  sana ila Mungu kampenda zaidi yetu  hivyo hatunabudi kusema jina lake  lihimidiwe milele yote




Chanzo;Fransis godwin blog

INASIKITISHA SANAA WATOTO WAWILI WAFUNGIWA NDANI MIEZI SITA (6) WADAI HAWATAUSAHAU MWAKA 2013

 
“TUNAJUA shangazi anatutesa kwa sababu baba na mama wapo mbali, kama wangekuwepo hapa tusingeteswa hivi. Tunamuomba baba, tunamuomba mama kama watasoma habari hii waje watuchukue turudi nyumbani, shangazi anatutesa sana, wala hatukutegemea,” ndivyo alivyoanza kusema mtoto Hassan Yusuf (5) ambaye ni mkubwa kwa wenzake, Hussein Yusuf (5) na Rehema Said (5).

Ikifika mahali mtoto mdogo anasema anawakumbuka wazazi wake kwa sababu ya mateso anayoyapata ugenini ujue ni zaidi ya ukatili, tena ni ukatili wa kutisha.
Watoto hao, kwa sasa wanaishi Nzasa ‘A’, Kata ya Charambe, Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam na ndiko walikopatia mateso yote. 

MAMBO YALIPOANZA KUTIBUKA
Wiki iliyopita, watoto hao waliokolewa na majirani katika kifungo cha miezi sita ndani huku afya zao zikiwa zimedhoofu kwa kukosa chakula. 

Ilidaiwa kwamba, watoto hao Hassan na Hussein ambao ni mapacha na Rehema,  walifungiwa katika banda la shangazi yao aitwaye Asia Bora ambalo ujenzi wake haujakamilika. Wamekuwa wakiishi humo kwa kula mabaki ya vyakula jalalani. 

USHUHUDA WA MAJIRANI
Wakizungumza na gazeti hili hivi karibuni, majirani wa nyumba hiyo walimweleza mwandishi wetu  kuwa watoto hao wamekuwa wakionekana  nje ya nyumba hiyo mara chache sana wakiwa wanagombania mabaki ya vyakula kwenye jalala. 

“Tumekuwa tukiwaona nje mara chache kwenye jalala. Unajua, Asia (shangazi yao) aliwachukua kwa kaka yake, Kijiji cha Namakongoro Kata ya Lihimalyao huko Kilwa mkoani Lindi.

“Tukasikia lengo lake aje kuishi nao kwa vile yeye Mungu hamkujalia kupata watoto. Lakini maisha hapo kwake yakawa siyo mazuri kwa kipato kwa mama huyo. 

Mmoja wa majirani hao aliyejitambulisha kwa jina la Aisha Ramadhan yeye alikwenda mbele zaidi kwa kusema:

“Hapo awali tulikuwa tukiwaona wakitoka nje na kucheza na watoto wetu huku wakiwa na afya nzuri. Asia akatueleza kuwa ni watoto wa nduguye, amewachukua huko kijijini. 

“Baada ya muda fulani tukawa hatuwaoni, tulidhani amawarudisha kwao, lakini kadiri siku zilivyokuwa zinakwenda mbele tukawa tunawaona mara chache wakiwa jalalani wanapigania mabaki ya chakula.

“Kuna siku mimi niliwakamata wakiwa wamebeba mfuko wa rambo wenye kinyesi, walikuwa wanakuja kutupa katika maeneo yetu, nikawarudisha nao kwa shangazi yao. Kumbe nyumba wanayoishi haina choo ndiyo maana wamekuwa wakijisaidia kwenye rambo. 

“Siku moja walipotoka nje kutafuta chakula jalalani, mimi na majirani wenzangu tuliwauliza wanaishije? Wakatuambia hawapewi chakula na shangazi yao akitoka asubuhi harudi mapema, akirudi inakuwa ni usiku sana wao wakiwa wameshalala. 

“Inasikitisha sana kuwaona watoto hawa wanaachwa peke yao kutwa nzima bila mtu wa kukaa nao na wamekuwa wakifungiwa ndani kwa muda mrefu sasa, ila huwa wanakiuka masharti na kutoka kwa ajili ya kutafuta mabaki ya chakula. 

Jirani huyo akaendelea kuanika mateso ya watoto hao: “Kwa kuwaonea huruma tumekuwa tukilazimika kuwapa chakula, lakini Asia anaporudi na kugundua hilo anawapiga, kwa hiyo wakawa waoga kuja kuchukua chakula. Mimi niliumia hadi machozi.” 

Jirani: “Baadaye wakawa hawaonekani, lakini cha ajabu mara nyingi tukiamka asubuhi tunakuta mifuko ya rambo yenye vinyesi imetapakaa, tukimweleza Asia inakuwa ugomvi.

“Siku moja baada ya shangazi yao kuondoka, nilikwenda kuwachungulia ndani, nikawaona wamekonda sana, wamepauka na wamevaa nguo zilizochakaa. 

“Nilitokwa machozi, nililazimika kuwaita wenzangu nao walipofika hakuna aliyejizuia kulia. Tukasema hawa watoto watakufa, ndiyo tukaamua kuwaokoa kwa kupeleka taarifa kwa mzee Dadi Salum ambaye ni polisi jamii wa hapa. 

POLISI JAMII NAYE ALIA
“Mzee Dadi naye alipofika na kuwaona kwa macho alilia, watu wakaanza kukusanyika, tukawatoa nje watoto, kila mmoja aliwaonea huruma. Tuliwachukua hadi Ofisi ya Serikali ya Mtaa wa Nzasa A. 

SHANGAZI MTU ANUSURUKA KIPIGO
“Hatujui ni nani aliyempigia simu Asia, kwani muda mfupi tu tukasikia yupo nyumbani kwake. Uongozi wa mtaa ulimfuata, walipofika, wanawake wenzake hasa wale anaochukua nao mkopo wa fedha benki walitaka kumpiga wakimuuliza pesa anapeleka wapi. 

“Hata hivyo aliokolewa na polisi jamii ambao walimchukua na kumweka katika Bajaj na kumpeleka Kituo cha Polisi Mbagala kwenye Dawati la Jinsia na Watoto, watoto nao pia walipelekwa huko.”

Naye Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Nzasa A, Mrisho Salum alikiri kuwapokea watoto hao wakiwa katika hali mbaya kiafya, wakapelekwa polisi. Akawataka wananchi kutokaa kimya mara wanapoona vitendo kama hivyo. 

Mwandishi alifika hadi kituo cha polisi na kuambiwa na askari mmoja kuwa mapacha walichukuliwa na mtu aliyejitambulisha kwa jina la Othman Mbwana  aliyedai ni babu yao.

Mbwana alidai kwamba ameamua kuwachukua watoto hao wakaishi nyumbani kwake wakati akifanya mawasiliano na wazazi wao.
“Kwanza nitawapeleka hospitali wakatazamwe afya zao, ila nimesikitishwa sana na hali hii, sijajua ni kwa nini watoto hawa wamefikia hatua hii,” alisema Mbwana.

Rehema yeye alichukuliwa na mjomba wake aitwaye Sood Ismail ambaye alidai anakwenda kukaa naye hadi hapo atakapofanya mawasiliano na wazazi wa huyo mtoto, akisema kitendo cha Asia kimeidhalilisha familia. 

RPC TEMEKE ATUPIA NENO
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Engelbert Kiondo amewataka wananchi kufichua vitendo viovu ndani ya jamii na amewapongeza vijana wake wa ulinzi shirikishi kuokoa maisha ya hao watoto.

Saturday, 28 December 2013

UJUE UKWELI KUHUSU DIAMOND....HAMNA WA KUCHEZA LIGI MOJA NAE SASA HIVI...!SOMA ZAIDI HAPA...

Ni msanii gani anayecheza ligi moja na Diamond Platnumz sasa hivi? Naamini yupo kwenye ligi yake mwenyewe na hadi sasa hana mpinzani. Japokuwa kama ni mpira wa miguu, Diamond anaweza kuwa kwenye ligi kuu pamoja na timu zingine (wasanii wenzie) kwa anachokifanya, anaweza kuwa kwenye ligi kuu plus ambayo hakuna msanii mwingine anayefikia matawi yake.
Kutoka kwenye historia ndefu iliyokumbwa na umaskini wa kutupa enzi za utoto na ujana wake kabla hajatusua, hadi kufikia kuwa msanii tajiri, anayetafutwa kuliko wote kwaajili ya show na anayelipwa fedha nyingi zaidi kuliko wote. Kutoka kwenye maisha ya kudhauliwa, kufanya kazi kwenye viwanda na ujira wa shilingi 3,000 kwa siku, hadi kuwa msanii anayeingiza si chini ya shilingi milioni 40 kila wiki. Hakuna msanii anayependwa zaidi nchini kwa sasa kumzidi. Pamoja na sifa nzuri za kuwa hitmaker maisha yake upande wa pili yamekuwa yakiandamwa na scandal nyingi. Amekuwa na uhusiano wa kimapenzi na wasichana wengi warembo na wenye majina ambao wengi wao ameishia kuwavunja roho kutokana na kutokuwa mwaminifu kwenye uhusiano wake. 
Japo anasema amewahi kuumizwa sana na Wema Sepetu aliyemtuhumu kwa kutokuwa mwaminifu katika uhusiano wao, Wema pia anasema amewahi kuumizwa mara nyingi na Diamond. Kwa maana nyingine ni kuwa, Diamond na Wema wana mambo mengi wanayofanana; wote ni heartbreakers. 
Wema na Diamond wamekuwa na uhusiano wa on and off kwa kipindi kirefu. Pamoja na wakati mwingine kila mmoja kuamua kuendelea na maisha yake, wapenzi hawa wameendelea kuhook up kisirisiri na kuendelea kulila tunda lao. Mara ya kwanza wameachana, Wema ndiye aliyemshutumu mwenzi kwa kumsaliti.
 clip_image001[8]

“Mimi na Naseeb tuliachana baada ya yeye kunicheat na Jokate,” Wema aliliambiagazeti la Mzuka katikati ya mwaka huu. “Nilikuwa sijui and maisha yangu yote tangianimeanzamapenzi na Naseeb naweza kusema kuwa sikuwahi kuwa unfaithful.
 I used to be very faithful to him na tulikuwa tunapendana sana. With Naseeb nilikuwa nimesharidhika na maisha ambayo niko nayo na hata kama yalikuwa not good, whatever lakini tayari nilikuwa nipo satisfied with me and him nilikuwa tayari nimesharidhika naye.
Nadhani pia inacost mwanaume akishajua kwamba anakutawala in one way or another so labda ni shetani au ni ibilisi alimuingilia baada ya kutaka kuanza kushoot video ya Mawazo ndo rumors zilianza, nikawa siamini kwanza. Siku moja ndio nikapigiwa simu na rafiki yangu anafanya kazi Piccolo akaniambia ‘Diamond yuko hapa na Jokate na wanakiss’. Nilitoka, nikachukua taxi nikaenda mpaka Piccolo, kitu cha kwanza niliona gari yake. Nilivyofika nikawakuta sijui wamewekeana miguu. Nilivyofika pale nikawasalimia wakawa wako kimya na nimeona ile kitu nikawaaga nikaondoka zangu. Nikaliaaaa, amerudi wakati huo bado tunaishi pamoja akanikutana napanga nguo, hakutaka kuongea sikutaka kuongea, tukachuniana, sikulala mimi na Naseeb kitandani for one week. Anaiona ile hali lakini hataki kuanza. Nikachoka, nikaja tu siku nimepanga nguo zangu nikaenda kwa dada yangu ndio ikawa kimoja. Basi mimi nikamwacha akaendelea na maisha yake na mimi nikaendelea na maisha yangu.” Kipindi Diamond anakutana na Jokate, mrembo huyo alikuwa tayari yupo kwenye uhusiano na mchezaji wa ligi ya NBA, Hasheem Thabeet. Uhusiano wao ulikuwa umedumu kwa miaka miwili na Jokate alikiri kuwa alikuwa akimpenda sana mchezaji huyo. Hata hivyo muda huo umbali wao na matatizo ya hapa na pale ukamfanya Jokate awe kwenye hali ya upweke na hivyo kumpa nafasi Diamond. clip_image001[6] 
“Kulikuwa na vitu vingi akatumia nafasi au fursa kama wanavyosema siku hizi. Ilitokea tu. Nilikuwa kwenye hali fulani akatumia nafasi hiyo lakini angenitongoza mwaka huu nisingemkubali,” Jokate aliliambia gazeti la Ijumaa Wikienda October mwaka huu.
Hata hivyo, Jokate alijikuta miongoni mwa wasichana wengi waliyoumizwa na Diamond baada ya kuwa naye kwa kipindi cha miezi miwili tu.
Kupitia kipindi cha Take One cha Clouds TV, cha katikati ya mwaka huu, Diamond alikiri kumuuliza Jokate.
“Kwasababu alikuwa too innocent halafu hakuwahi kunikosea kitu chochote Jokate kabisa, halafu nikamwingiza kwenye matatizo, watu wakamchukulia tofauti kwamba ‘Jokate kamchukulia Wema boyfriend wake’ wakati nilimfuata mimi kama mimi, nilimtafuta mwenyewe halafu then nikawa niko naye halafu ghafla nikarudisha mahusiano kwa Wema. Sikujiskia vizuri halafu still haikuwa vizuri so sometimes nikikaaga hivi nasema nilimkosea,” alisema Diamond.
Akijibu swali la kwanini alimuacha Jokate, Diamond aliongeza, “Sijui nilirogwa hata sijui, I don’t know, sijui hata kwanini, hakuwahi kunikosea chochote sio, sababu nilikuwa nikikaa naye alikuwa akinishauri vitu vingi vya maendeleo, sijui ulikuwa ni utoto sielewi yaani, sijui ni kitu gani, nilijikisa vibaya sana, halafu mtoto wa watu mstaarabu sana, alijitahidi kujenga career yake sasa hivi imekaa vizuri.”
Bongo5 iliwasiliana na Jokate ili kutaka kufahamu upande wake baada ya kusikia kauli ya Diamond na kusema anafurahi kuona Diamond amefunguka ukweli. “Watu wengi hawajui the real issue, I’m glad kama ame-acknowledge I was innocent in that whole matter,” alisema Jokate.
Pamoja na kuachana huko kulikoonesha ishara ya kutorudiana tena, Diamond na Wema waliendelea kuwa na ukaribu ambao kwa kiasi kikubwa ulikuwa ukiwaumiza wengi. Msichana aliyekuja kuumizwa zaidi ni Penny ambaye kwake Diamond alikuwa mwanaume wa kipekee. clip_image001 
“Lakini I will tell you one thing, Diamond is an amazing person, whatever you see anachofanya, whether he is kissing, he is talking to me, whether ananichekesha, yaani he is a five star. So you can imagine ilikuaje. It was weird but very good; everything about him is just amazing,” Jokate aliliambia jarida la Mzuka.
Aliliambia jinsi ambavyo Diamond alikuwa akimfanyia surprise nyingi na mapenzi tele.
“The first one I think is buying me a car coz sikuexpect, I didn’t see it coming, ilikuwa out of the blue. Unajua tumeshazoea kwamba watu wanaofanya vitu hivi ni wanaume wakubwa, wababa mpaka uhongwe umehongwa na mtu mzima lakini for Diamond amesema hivyo tu ghafla…. nilikuwa sijui natoka naenda wapi akaniambia hebu njoo nikuambie he said, ‘I got you a car, he gave me money akasema go and buy that car,” alisema na kuongeza kuwa Diamond alimkabidhi shilingi milioni 15 kununua gari hilo.
“He said go buy this car. Ananiulizaga, he is very funny’ unapenda gari fulani mi’ mimi najibu yeah I like it’. I was so shocked, ghafla so I think that’s the first surprise. He is too sweet; kwanza he will come take you out for a dinner out of the blue. Yaani anafanya vitu ambavyo kwa age yake na persona yake vilivyo alivyo an artist unategemea awe ghetto, ‘ebwana uko wapi twenzetu pale tukapige kiepe’ unajua vile. But he is very sweet that surprises me, he surprises me I think every day. Na anachonisurprise kingine kikubwa I will tell you guys, ni uwezo wake wa kufikiri, he is very smart.”  
Bahati mbaya kuamini huko kumekuja kugeuka baada ya hivi karibuni Diamond kurudiana na Wema Sepetu na ukweli huo ulibainika baada ya kuvuja picha zao wakiwa Hong Kong hivi karibuni. Tukio hilo liliuvunja vibaya moyo wa Penny ambaye tayari alikuwa akiishi na Diamond na nyumbani kwao alikuwa akijulikana na mchumba aliyepitishwa na familia nzima akiwemo mama yake Diamond na dada zake.
Usaliti huo ulipelekea mgogoro mkubwa kati ya Diamond na Penny ambaye kuna tayari kuna tetesi kuwa wameshaachana rasmi. Tangu hapo Wema amekuwa haoni aibu kuonesha mapenzi yake kwa Diamond ikiwa ni pamoja na kupromote show ya Diamond ya Christmas.
Kwenye show hiyo ya Jumatano hii ndipo mambo yalipowekwa wazi zaidi ambapo Wema alikuwa mmoja wa watu waliopanda kwenye stage na kuongea na watoto waliokuwa wakishuhudia show. Kwenye show hiyo Diamond alisikika akiuliza: Mnataka kumjua mchumba wangu”? Baadaye wakati akitaka kuimba wimbo wake ‘Ukimwona’, hitmaker huyo aliuliza tena: Naskia ninayetaka kumuimbia wimbo huu yupo humuhumu ndani,” na ndipo Wema Sepetu akapanda kwenye stage wakaimba na kucheza wote.
Baada ya Penny, hatujui ni msichana gani atakayevunjwa tena moyo na Diamond kutokana na kuendelea kwa uhusiano usiokatika na Wema kama vile wamekula yamini

MAN UNITED WAZIDI KUPANDA KATIKA MSIMAMO WA LIGI KUU ENGLAND

NORWICH 0 MAN UNITED 1WALBECKDanny Welbeck, akitokea Benchi na kuingizwa Kipindi cha Pili, aliifungia Man United Bao 1 na la ushindi huko Carrow Road na kuitungua Norwich City Bao 1-0.

[WALBECK%255B3%255D.jpg]

Meneja wa Man United, David Moyes, leo alibadilisha Wachezaji watano toka Kikosi kilichoifunga Hull City 3-2 Juzi kwa kuwachezesha Nemanja Vidic, Michael Carrick, ambae hii ilikuwa Mechi yake ya kwanza tangu Oktoba, Ryan Giggs, Shinji Kagawa na Javier Hernandez huku Wayne Rooney akikosekana kabisa.

Huu ni ushindi wa nne mfululizo kwenye Ligi na umewapaisha hadi Nafasi ya 6 kwenye Msimamo.

VIKOSI: Norwich: Ruddy, Martin, Ryan Bennett, Bassong, Olsson, Johnson, Fer, Snodgrass, Hoolahan, Redmond, Hooper. Subs: Whittaker, van Wolfswinkel, Bunn, Elmander, Garrido, Becchio, Murphy.

Man United: De Gea, Smalling, Evans, Vidic, Evra, Young, Cleverley, Carrick, Giggs, Kagawa, Hernandez. Subs: Anderson, Lindegaard, Welbeck, Fabio Da Silva, Fletcher, Zaha, Januzaj.

MAN CITY 1 CRYSTAL PALACE 0 DZEKOEdin Dzeko aliifungia Man City Bao moja na pekee walipocheza na Crystal Palace Uwanjani Etihad na kuwafanya wachukue uongozi wa Ligi wakiwa Pointi 2 mbele ya Arsenal.



[DZEKO%255B3%255D.jpg]

VIKOSI: Man City: Hart, Boyata, Kompany, Nastasic, Clichy, Fernandinho, Javi Garcia, Jesus Navas, Silva, Milner, Dzeko

Akiba: Lescott, Nasri, Negredo, Kolarov, Rodwell, Pantilimon, Toure.

Crystal Palace: Speroni, Delaney, Mariappa, Gabbidon, Parr, Puncheon, Ward, Bannan, Jedinak, Bolasie, Jerome

Akiba: Campana, Phillips, Gayle, Jonathan Williams, Moxey, Chamakh, Price.

Refa: Andre Marriner

ASTON VILLA 1 SWANSEA 1ROLAND

Aston Villa leo wamemaliza wimbi lao la kufungwa Mechi 4 mfululizo za Ligi kwa kutoka Sare ya 1-1 na Swansea City Uwanjani Villa Park.

[ROLAND%255B3%255D.jpg]

AGBONLAHOR Villa ndio waliotangulia kufunga kwa Bao la Gabriel Agbonlahor la Dakika ya 7 na Swansea kusawazisha katika Dakika ya 36 kwa Bao la Roland Lamah.

VIKOSI: Aston Villa: Guzan, Lowton, Baker, Clark, Luna, Bacuna, Westwood, Delph, Weimann, Agbonlahor, Tonev.

Akiba: El Ahmadi, Helenius, Albrighton, Steer, Sylla, Bowery, Kozak.

Swansea: Tremmel, Tiendalli, Chico, Williams, Ben Davies, de Guzman, Canas, Hernandez, Shelvey, Lamah, Bony.

Akiba: Amat, Britton, Routledge, Rangel, Pozuelo, Vazquez, Zabret.

Refa: Roger East

HULL 6 FULHAM 0TOM HUDDLESTONE

Hull City, wakiwa kwao KC Stadium, leo wameifumua Fulham Bao 6-0 huku Bao zote zikifungwa Kipindi cha Pili.


[AGBONLAHOR%255B3%255D.jpg]

Bao za Hull City zilifungwa na Ahmed Elmohamady, Robert Koren, Bao 2, George Boyd, Huddlestone na Matty Fryatt.

VIKOSI: Hull: McGregor, Rosenior, Chester, Davies, Figueroa, Elmohamady, Livermore, Koren, Huddlestone, Boyd, Sagbo

Akiba: Bruce, Meyler, Graham, Fryatt, McShane, Harper, Faye.

Fulham: Stockdale, Zverotic, Hughes, Amorebieta, Riise, Sidwell, Karagounis, Dejagah, Kasami, Ruiz, Rodallega

Akiba: Kacaniklic, Richardson, Boateng, Riether, David, Bent, Bettinelli.

MWAMVITA MAKAMBA AFUNGUKA ADAI NI BORA KUVULIWA NGUO NA WANAUME ILA SIO KUUZA MADAWA YA KULEVYA


 
 Adai ni bora ukavuliwa nguo na mwanaume kuliko kuuza unga
 

BALAAA MAHARI YASABABISHA NDOA ISIFUNGWE , WAUMINI NA MCHUNGAJI WAKAA KANISANI WASIJUE LA KUFANYA

Bwana Harusi Fadhili Mahenge akiwa ndani ya Suti akisubiri kufungishwa ndoa 

Bi Harusi Naomi Ngoje akiwa amejilalia chumbani akisubiri hatima ya Wazazi ndipo ajiandae kwenda kanisani tayari kwa kufunga ndoa na mchumba wake waliodumu kwa miezi saba.
Bwana harusi akiwa na mpambe wake kanisani wakimsubiri bibi Harusi
Askofu Kenani Mpalala akiwa katika picha ya pomaja na Bwana Harusi na mpambe wake muda mfupi baada ya kuwasili kanisani
Askofu Keenan Mpalala wa kanisa la Free Pentecost Church of Tanzania akionesha tangazo la Ndoa
Baadhi ya ndugu wa mwanamke wakiwa katika kikao na kuendelea na msimamo wao kuwa mahali lazima imalize ndipo wamtoe binti yao
Jamaa wameshika vichwa hali haieleweki

Baadhi ya akina mama wakiangalia ratiba ya harusi
Kanisani
Baadhi ya waumini na majirani wakisubiri kanisani




KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida Familia moja ya Makunguru  Mtaa wa Ilolo Jijini Mbeya imesababisha sintofahamu dhidi ya Familia nyingine baada ya kumkatalia binti yao kuolewa kwa madai ya waoaji kutokamilisha Mahari waliyokuwa wamepangiwa.

Tukio hilo la aina yake limetokea leo ambapo Bwana harusi aliyefahamika kwa jina la Fadhili Mahenge(28) Mkazi wa Songea aliyekuwa amuoe Naomi Ngoje na harusi yao kufungwa katika kanisa la Free Pentecoste Church Of Tanzania(FPCT) lililopo Makunguru Jijini hapa kushindwa kufungwa baada ya wazazi wa Bibi harusi kuzuia ndoa hiyo hadi Mahari itakapokamilika.

Wakizungumzia tukio hilo Nyumbani kwa Familia ya Bibi Harusi, Mjomba wa Bibi Harusi Dickson Ngoje amesema tatizo la wao kugomea ndoa hiyo ni kutaka waoaji kutimiza masharti waliokuwa wamekubaliana awali ambayo hadi siku ya mwisho familia hiyo haijatekeleza.

Amesema siku ya kwanza waoaji walifika Nyumbani kwa Mzee Ngoje na kujitambulisha ambapo walipangiwa taratibu za mahari kwa mujibu wa Mila kuwa watatakiwa kutoa Blanket 2, Mashuka mawili, Mkaja(200,000), mbuzi 4, Majembe 4, Ng’ombe Jike 2 na Ngo’mbe Dume 1 pamoja na fedha taslimu Shilingi Laki 3.

Amesema baada ya Familia hiyo ya Waoaji ambao ni Ukoo wa Mahenge kupangiwa vitu hivyo waliondoka na kuahidi kurudi siku nyingine kwa ajili kukamilisha vitu walivyopangiwa ambapo walirudi Septemba 11, Mwaka huu wakiongozwa na Mshenga aliyejulikana kwa jina moja la Mzee Katete wakiwa na Blanketi 2, Mashuka mawili pamoja na Fedha shilingi 10,000/= ambazo walizipokea na kuwaambia hawawezi kuzungumza chochote juu ya Ndoa.

Mjomba huyo anaongeza kuwa baada ya wiki mbili familia hiyo ilirudi na kukuta Nyumbani kuna ukoo mzima wakiwa na Shilingi 200,000/= ndipo walipoambiwa walipe kiingilio shilingi 100,000/= ndiyo wanaweza kupokelewa nyumbani jambo ambalo walilitekeleza kisha kulipa fedha walizokuwa nazo kama Mkaja na kuomba wapewe kibali cha kuandikisha ndoa na taratibu za kumalizia vilivyobaki zikiendelea.

Anasema tangu hapo Ndoa ilianza kutangazwa Disemba 8 na kuisha Disemba 22, Mwaka huu baada ya kutangazwa mara tatu huku tangazo likiashiria ndoa kufungwa tarehe 28/12/2013 ambapo wazazi wakiahidi kumalizia Mahari iliyobaki kabla ya siku ya kufunga ndoa.

Akizungumzia kwa kirefu kashishe hiyo, Mjomba huyo anasema baada ya wazazi wa Mwanaume kusisitiza kumaliza kila kitu hadi ifikapo Disemba 23, Mwaka huu na wao walijikusanya na kupanga taratibu za sherehe hususani ya kumwaga binti yao(Send Off) ambayo ilifanyika Disemba 24, Mwaka huu.

Aidha baadhi ya ndugu wameongeza kuwa familia hiyo haioneshi uaminifu wa kumalizia Mahari hiyo kutokana na ahadi zisizotekelezeka walizotoa tangu kipindi cha nyuma na kuongeza kuwa hata kwenye sherehe ya kumwaga binti yao walifika baadhi ya ndugu wakiwa na Zawadi tofauti na taratibu zinavyotaka.

Wamesema kwa mujibu wa taratibu za Sherehe za SendOff upande wa Mwanaume unatakiwa kuleta zawadi ambazo ni  nguo za Bibi Harusi za kuvaa siku ya Ndoa Pamoja n Harusi lakini wao hawakufanya hivyo ingawa walikuwa na Nguo ambazo tayari zilikuwa zimetumika.

Kwa upande wa Mchungaji aliyekuwa anataka kufingisha Ndoa hiyo ambaye pia ni Askofu wa Kanisa hilo, Mchungaji Kenan Mpalala alipoulizwa kuhusu hali hiyo amesema kwa mujibu wa taratibu za Sheria ya Ndoa ya mwaka 1971 kifungu cha 8 pingamizi litolewe ndani ya siku 21.

Amesema upande wa Wazazi wa Mwanamke ulishindwa kuwasilisha pingamizi lao kanisani kabla ya Siku 21 badala yake walifika kutoa malalamiko kuhusu kutomaliziwa kwa mahali jambo ambalo alisema yeye kama Mwandikisha Ndoa halimhusu bali pande mbili wanatakiwa kulimaliza kabla ya Ndoa.

Naye Bwana Harusi Mtarajiwa Fadhili Mahenge(28) alipoulizwa kuhusiana na suala hilo huku akiwa tayari Kanisani kwa ajili ya Kufungishwa Ndoa alisema anachosubiri ni hatma ya Wazazi wa Mwanamke kama wanaweza kumwachia Mkewe iliwanachodai awe anamalizia taratibu.

Amesema yeye kama yeye kwa sasa hana fedha zozote za kuweza kumalizia anachodaiwa zaidi ya kuomba busara za wazazi wa Mwanamke kumruhusu Ndoa ifungwe ndipo aweze kulipa Mahari anayodaiwa kwa awamu kutokana na hali yake ya kiuchumi kuwa Mbaya.

Ameenda mbali zaidi kwa kusema kama Wazazi wa Mwanamke wataendelea kuwa na Msimamo huo basi hata yeye ataomba arudishiwe kile alichokitoa awali ili ajipange upya kwa ajili ya ndoa baada ya kukamilisha madai yao.

Hadi tunaingia mtamboni Mbeyayetu ambayo ilikuwepo sehemu ya tukio timu ya usuluhishi ilikuwa ikiendelea na kazi yake ikiongozwa na Mchungaji, Mwenyekiti wa Mtaa na Mzee Maarufu ambaye ni Katibu wa Chama cha Wakulima (TASO) kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Ramadhani Kiboko, huku muafaka ukiwa haujapatikana.
Na Mbeya yetu

Friday, 27 December 2013

HII NI BALAAA SANA JAMAA AFUMWA NA KIMADA AKIVUNJA AMRI YA SITA NDANI YA GARI


 

KRISMASI noma sana! Mwanaume aliyefahamika kwa jina la Baba Pendo ameiona chungu Sikukuu ya Krismasi 2013 kufuatia tukio la kufumaniwa na mkewe, Mama Pendo au Mama P ‘akibanjuka’ na mwanamke ndani ya gari. 

NI MKESHA WA KRISMASI
Tukio hilo la aina yake lilijiri eneo maarufu Kijitonyama jijini Dar linalojulikana kwa jina la Miti Mirefu, usiku wa Mkesha wa Krismasi, majira ya saa 8:00 usiku wa kuamkia Jumatano iliyopita.
Ina maana kwamba Baba Pendo aliamua ‘kumalizia shida’ zake ndani ya gari hilo ambalo namba zake za usajili tunaziweka kapuni.

 
OFM YAJUZWA
Kabla ya tukio hilo, mara kadhaa Mama P aliwasiliana na Oparesheni Fichua Maovu (OFM) ya Global Publishers na kulalamika juu ya mumewe kutoka nje ya ndoa na mwanamke mmoja wa mjini.
Mama P: Haloo…naongea na OFM? Jamani naombeni mnisaidie kuna mwanamke anamzuzua sana mke wangu.
OFM: Una uhakika mama?

Mama P: Nina uhakika wa asilimia mia moja. Hapa nimeona meseji wamepanga kukutana leo na ndiyo maana nikawatafuta. Ninyi mpo wapi?
OFM: Sawa, sisi tupo kikazi Mango Garden (Kinondoni, Dar) wewe upo wapi?
Mama P: Nipo Sinza A (Dar) nitawashtua mambo yakiiva maana najua lazima mume wangu atatoka muda si mrefu, nimemuona anajiandaa.

OFM: Oke lakini uwe makini sana.
Mama P: Sawa, nitawashtua.
Hiyo ilikuwa saa 5:12 usiku, hivyo OFM iliendelea na majukumu mengine ya kufichua uovu katika jamii.

 
BABA PENDO AAGA ANAKWENDA MKESHA
Kwa mujibu wa Mama P, majira ya saa 5:20 usiku, mumewe alimuaga anakwenda kwenye mkesha wa kumpokea mwana wa Mungu (Yesu) aliyezaliwa ambapo kwa mujibu wa mume huyo, alikuwa anakwenda kusali Kanisa la Mtakatifu Maximilian Kolbe lililopo Mwenge, Dar.

 
MAMA P MZIGONI
Baada ya mumewe kuondoka, mwanamke huyo aliwasiliana na OFM na kuwapa ishu nzima ambapo walimpa mbinu ya kumfuatilia mumewe ikiwa ni pamoja na kubadili aina ya usafiri ili asishtuke.

Mama P alichukua Bajaj na kumfuatilia mumewe hadi maeneo ya Sinza-Kijiweni ambapo alimuona akipaki gari lake na kuingia kwenye ‘pabu’ moja kisha akaagiza ‘ngumu kumeza’ (mzinga wa konya) ambayo aliipiga taratibu hadi mishale ya saa 8: 05 usiku huku akipiga stori na washkaji.
Baada ya hapo, Baba Pendo aliingia garini kuondoka. Mama P naye akachukua bodaboda kumfuatilia kwa nyuma.
Alipofika maeneo ya Kijitonyama  alimuona akisimamisha gari na kuingia kwenye ‘kamtaa’ f’lani, akatoka na mwanamke kisha akaingia naye kwenye gari.
Alisema yeye akiwa bado nyuma, walipofika Miti Mirefu  mumewe alipaki gari lakini hakuna aliyeshuka.

Aliendelea kusimulia kisa mkasa mbele ya ‘kachero’ wa OFM kuwa uvumilivu ulimshinda, alihisi kuna linaloendelea ndani ya gari,  akaamua kulisogelea na ndipo hamadi! Akamkuta mumewe ‘laivu akiduu’ na mwanamke huyo na ndipo OFM walipochomoza baada ya kujulishwa kuwa ishu imetiki.
“Uzuri ni kwamba walisahau ‘kuloki’ milango ya gari ‘so’ nilipoushika ukafunguka,” alisema Mama P baada ya OFM kupiga picha za kutosha.

 
TIMBWILI
Katika tukio hilo kulitokea timbwili ambapo askari waliokuwa doria walitonywa na kufika eneo la tukio na kuamulia damu isimwagike.
Mwanamke aliyenaswa na mume wa mtu alikula mbata za kufa mtu huku mwanaume akitoka nduki kukwepa aibu ya kamera za OFM.

 
MAMA P HASIRA
OFM ilimsikia Mama P akisema: “Kumbe ndiyo wewe…nilikuwa nakufuatilia muda mrefu, badala ya kwenda kanisani unahangaika na waume za watu hata humuogopi Mungu.”

Hadi gazeti hili linaondoka eneo la tukio, wanawake hao walikuwa mikononi mwa polisi wakitakiwa kuacha ugomvi na kama kuna malalamiko wayafikishe kituoni.GPL:

MSANII MENINA AFUNGUKA ADAI "SIWEZI KUTOA RUSHWA YA NGONO ILI NITOKE KIMUZIKI"

 
MWANAMUZIKI aliyeibukia kwenye Shindano la Epiq Bongo Star Search 2012, Menina Atick amesema licha ya kusikia kuwepo kwa baadhi ya wanaume wenye nafasi kwenye ‘game’ la muziki ambao huomba rushwa ya ngono kwa wasanii wa kike ili wawatoe, yeye atakomaa na anaamini atasimama.Akizungumza na Ijumaa hivi karibuni Menina ambaye sasa anasumbua na wimbo wake



wa Shaghala Baghala alisema anachoamini ni kwamba msanii wa kike mwenye kipaji hata asipotoa rushwa ya ngono, nafasi ya kung’ara anayo, hivyo yeye atakuwa mfano kwa wengine.
“Mimi…nitoe rushwa ya ngono ili nitoke, mh…kwa kweli hiyo haiwezekani, najiamini na sitakubali kuutumia mwili wangu kwa kugawa penzi ili nisimame kwenye muziki, kwanza

Saturday, 21 December 2013

HUYU NDO MSANII ANAEDAI HAJAWAHII KUDO MWAKA HUU MTAZAME HAPA


 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
Ni miongoni kati ya mastaa wanaotisha kwenye Tasnia ya Filamu hapa bongo Salma Jabu ‘Nisha’ aliyewahi kuingia kwenye game la muziki kwa kufuata mkumbo. 
‘Nisha’ now katia fora kwa kumaliza mwaka kishujaa bila ya kuwa na 
 
mpenzi yeyote wala kushiriki tendo la ndoa ikiwa tangu alipoachana na mpenzi wake ambaye hakupenda kumtaja jina ni kutokana na busy aliyokuwa nayo mwaka 2013.
“Sikuweza kukaa na kufikiria suala la mapenzi kutokana na u-busy niliokuwanao tangu nilipoachana na mpenzi wangu lakini busy yangu ya kazi pia ndio ilionipa mafanikio niliyonayo hivyo namshukuru Mungu kwa kunilinda mwaka mzima “- Nisha.

SIMBA YAICHAKAZA YANGA BAO TATU KWA MOJA (3-1) UWANJA WA TAIFA DAR ES SALAAAM


 Hatimaye mpira umeisha na Simba watoka kifua mbele kwa bao 3- 1 ambalo limefungwa na okwi 

MUME AKIMBIA UCHI NI BAADA YA KUFUMANIWA GUEST NA MKE WAKE NI BALAAA SOMA ZAIDI

 
DUNIA ina mambo jamani! Mfanyabiashara wa madini aliyefahamika kwa jina moja la Jimmy amejikuta katika wakati mgumu baada ya kufumaniwa na mkewe akiwa na kimada gesti.
Tukio hilo lililofunga mtaa kwa kujaza wambea kibao, lilitokea hivi karibuni ndani ya gesti hiyo (jina tunalo) Kinondoni jijini Dar es salaam ambapo mke wa mfanyabiashara huyo (jina halikupatikana mara moja), alimnasa mumewe  akijiandaa kuvunja amri ya sita ya Muumba.


Mke wa mfanyaiashara (kulia) baada ya kumfumania kimada akiwa na mumewe gesti maeneo ya Kinondoni, jijini Dar.


Wadakuzi waliokuwa eneo la balaa walitonya kuwa, siku hiyo ya tukio, Jimmy ambaye ni mkazi wa jijini Arusha, alifika Dar kibiashara na baadaye alimsaka kimada huyo wa siku nyingi na kwenda kujirusha naye bila kujua mkewe alishatonywa juu ya usaliti wake.

Awali chanzo makini kinachojua nini maana ya habari kiliwatonya mapaparazi wetu mara baada ya kupata mchongo wa fumanizi kutokea Sinza ya Kumekucha lililoandaliwa na mke wa Jimmy.

“Nyie njooni tu hapa Sinza-Kumekucha ndipo mkewe alipotonywa na dereva wa mumewe kuwa anaibiwa na kimada. Kuna gesti moja ipo ndani kidogo upande wa kushoto kama unaelekea Shekilango,” kilisema chanzo.


Timu ya mapaparazi ilifika katika gesti hiyo lakini bahati mbaya waliambiwa kuwa, Jimmy na kimada huyo walihamisha kiwanja cha starehe na kwenda Kinondoni.


 

                                               Kimada aliyefumaniwa na mume wa mtu.

Mapaparazi walipofika katika gesti hiyo ya Kinondoni, walimkuta mke wa Jimmy hivyo wakaambatana naye pamoja na askari polisi wawili kwa ajili ya kwenda kufumania.


Jimmy kabla ya kuingia gesti inadaiwa alijipumzisha katika grosari iliyo karibu na Mango Garden Bar, baadaye akaenda kwenye gesti hiyo ya jirani bila kujua mkewe alikuwa akitua mguu kila pale yeye aliponyanyua, akazama ndani ya gesti hiyo na kuanza kujiandaa kwa zinaa.


Mke wa Jimmy hakuwa mbali, baada ya kujiridhisha mumewe amezama chumbani, dakika kadhaa na yeye alitokea na kugonga mlango wa chumba hicho kufuatia kutonywa na mhudumu mmoja wa gesti hiyo.

Jimmy alikutwa tayari ameshavua nguo zote na kubakiwa na ‘boksa’ huku kimada naye akiwa na ‘kufuli’ pekee.


Kilichofuata hapo ni kipigo, mke wa Jimmy alianza kumtembezea kipigo yule kimada. Mapaparazi walivamia na kutandika picha za timbwili ambapo Jimmy alifanikiwa kupenya mlangoni na kukimbia bila kujali nguo nyingine.

Kutokana na kelele za timbwili hilo, majirani wa eneo hilo walifika kuhoji kulikoni ambapo mfumaniaji huyo alitoboa siri kwamba amekuwa akimfuatilia mumewe kwa siku nyingi baada ya kuambiwa ana kimada Dar.


“Huyo malaya akome kutembea na waume za watu. Nimekuwa nikimfuatilia mume wangu kwa muda mrefu. Nimetoka Arusha mpaka Dar kwa ajili yake. Kweli za mwizi ni arobaini, leo nimewanasa,” alisema mwanamke huyo huku akiondoka eneo la tukio na kutokomea kusikojulikana.

Wakati pakichimbika, kimada huyo alisikika akimlaumu Jimmy kwamba amemuingiza kwenye mkenge akijua mkewe ni mdodosaji wa mambo na anaweza kufika Dar madai ambayo hayakuwa na wa kuyajibu.

Taarifa zaidi zilidai kuwa ndugu mmoja wa mwanamke huyo ndiye aliyekuwa na mchoro mzima wa Jimmy na hivyo ‘kuuza’ kwa mwanamke huyo.

credit: GPL