Ni
msanii gani anayecheza ligi moja na Diamond Platnumz sasa hivi? Naamini
yupo kwenye ligi yake mwenyewe na hadi sasa hana mpinzani. Japokuwa
kama ni mpira wa miguu, Diamond anaweza kuwa kwenye ligi kuu pamoja na
timu zingine (wasanii wenzie) kwa anachokifanya, anaweza kuwa kwenye
ligi kuu plus ambayo hakuna msanii mwingine anayefikia matawi yake.
Kutoka
kwenye historia ndefu iliyokumbwa na umaskini wa kutupa enzi za utoto
na ujana wake kabla hajatusua, hadi kufikia kuwa msanii tajiri,
anayetafutwa kuliko wote kwaajili ya show na anayelipwa fedha nyingi
zaidi kuliko wote. Kutoka kwenye maisha ya kudhauliwa, kufanya kazi
kwenye viwanda na ujira wa shilingi 3,000 kwa siku, hadi kuwa msanii
anayeingiza si chini ya shilingi milioni 40 kila wiki. Hakuna msanii
anayependwa zaidi nchini kwa sasa kumzidi. Pamoja
na sifa nzuri za kuwa hitmaker maisha yake upande wa pili yamekuwa
yakiandamwa na scandal nyingi. Amekuwa na uhusiano wa kimapenzi na
wasichana wengi warembo na wenye majina ambao wengi wao ameishia
kuwavunja roho kutokana na kutokuwa mwaminifu kwenye uhusiano wake.
Japo
anasema amewahi kuumizwa sana na Wema Sepetu aliyemtuhumu kwa kutokuwa
mwaminifu katika uhusiano wao, Wema pia anasema amewahi kuumizwa mara
nyingi na Diamond. Kwa maana nyingine ni kuwa, Diamond na Wema wana
mambo mengi wanayofanana; wote ni heartbreakers.
Wema
na Diamond wamekuwa na uhusiano wa on and off kwa kipindi kirefu.
Pamoja na wakati mwingine kila mmoja kuamua kuendelea na maisha yake,
wapenzi hawa wameendelea kuhook up kisirisiri na kuendelea kulila tunda
lao. Mara ya kwanza wameachana, Wema ndiye aliyemshutumu mwenzi kwa
kumsaliti.
“Mimi
na Naseeb tuliachana baada ya yeye kunicheat na Jokate,” Wema
aliliambiagazeti la Mzuka katikati ya mwaka huu. “Nilikuwa sijui and
maisha yangu yote tangianimeanzamapenzi na Naseeb naweza kusema kuwa
sikuwahi kuwa unfaithful.
I used to be very faithful to him na tulikuwa tunapendana sana. With Naseeb nilikuwa nimesharidhika na maisha ambayo niko nayo na hata kama yalikuwa not good, whatever lakini tayari nilikuwa nipo satisfied with me and him nilikuwa tayari nimesharidhika naye.
I used to be very faithful to him na tulikuwa tunapendana sana. With Naseeb nilikuwa nimesharidhika na maisha ambayo niko nayo na hata kama yalikuwa not good, whatever lakini tayari nilikuwa nipo satisfied with me and him nilikuwa tayari nimesharidhika naye.
Nadhani
pia inacost mwanaume akishajua kwamba anakutawala in one way or another
so labda ni shetani au ni ibilisi alimuingilia baada ya kutaka kuanza
kushoot video ya Mawazo ndo rumors zilianza, nikawa siamini kwanza. Siku
moja ndio nikapigiwa simu na rafiki yangu anafanya kazi Piccolo
akaniambia ‘Diamond yuko hapa na Jokate na wanakiss’. Nilitoka,
nikachukua taxi nikaenda mpaka Piccolo, kitu cha kwanza niliona gari
yake. Nilivyofika nikawakuta sijui wamewekeana miguu. Nilivyofika pale
nikawasalimia wakawa wako kimya na nimeona ile kitu nikawaaga nikaondoka
zangu. Nikaliaaaa, amerudi wakati huo bado tunaishi pamoja akanikutana
napanga nguo, hakutaka kuongea sikutaka kuongea, tukachuniana, sikulala
mimi na Naseeb kitandani for one week. Anaiona ile hali lakini hataki
kuanza. Nikachoka, nikaja tu siku nimepanga nguo zangu nikaenda kwa dada
yangu ndio ikawa kimoja. Basi mimi nikamwacha akaendelea na maisha yake
na mimi nikaendelea na maisha yangu.”
Kipindi
Diamond anakutana na Jokate, mrembo huyo alikuwa tayari yupo kwenye
uhusiano na mchezaji wa ligi ya NBA, Hasheem Thabeet. Uhusiano wao
ulikuwa umedumu kwa miaka miwili na Jokate alikiri kuwa alikuwa
akimpenda sana mchezaji huyo. Hata hivyo muda huo umbali wao na matatizo
ya hapa na pale ukamfanya Jokate awe kwenye hali ya upweke na hivyo
kumpa nafasi Diamond.
“Kulikuwa
na vitu vingi akatumia nafasi au fursa kama wanavyosema siku hizi.
Ilitokea tu. Nilikuwa kwenye hali fulani akatumia nafasi hiyo lakini
angenitongoza mwaka huu nisingemkubali,” Jokate aliliambia gazeti la
Ijumaa Wikienda October mwaka huu.
Hata
hivyo, Jokate alijikuta miongoni mwa wasichana wengi waliyoumizwa na
Diamond baada ya kuwa naye kwa kipindi cha miezi miwili tu.
Kupitia kipindi cha Take One cha Clouds TV, cha katikati ya mwaka huu, Diamond alikiri kumuuliza Jokate.
“Kwasababu
alikuwa too innocent halafu hakuwahi kunikosea kitu chochote Jokate
kabisa, halafu nikamwingiza kwenye matatizo, watu wakamchukulia tofauti
kwamba ‘Jokate kamchukulia Wema boyfriend wake’ wakati nilimfuata mimi
kama mimi, nilimtafuta mwenyewe halafu then nikawa niko naye halafu
ghafla nikarudisha mahusiano kwa Wema. Sikujiskia vizuri halafu still
haikuwa vizuri so sometimes nikikaaga hivi nasema nilimkosea,” alisema
Diamond.
Akijibu
swali la kwanini alimuacha Jokate, Diamond aliongeza, “Sijui nilirogwa
hata sijui, I don’t know, sijui hata kwanini, hakuwahi kunikosea
chochote sio, sababu nilikuwa nikikaa naye alikuwa akinishauri vitu
vingi vya maendeleo, sijui ulikuwa ni utoto sielewi yaani, sijui ni kitu
gani, nilijikisa vibaya sana, halafu mtoto wa watu mstaarabu sana,
alijitahidi kujenga career yake sasa hivi imekaa vizuri.”
Bongo5
iliwasiliana na Jokate ili kutaka kufahamu upande wake baada ya kusikia
kauli ya Diamond na kusema anafurahi kuona Diamond amefunguka ukweli.
“Watu wengi hawajui the real issue, I’m glad kama ame-acknowledge I was
innocent in that whole matter,” alisema Jokate.
Pamoja
na kuachana huko kulikoonesha ishara ya kutorudiana tena, Diamond na
Wema waliendelea kuwa na ukaribu ambao kwa kiasi kikubwa ulikuwa
ukiwaumiza wengi. Msichana aliyekuja kuumizwa zaidi ni Penny ambaye
kwake Diamond alikuwa mwanaume wa kipekee.
“Lakini
I will tell you one thing, Diamond is an amazing person, whatever you
see anachofanya, whether he is kissing, he is talking to me, whether
ananichekesha, yaani he is a five star. So you can imagine ilikuaje. It
was weird but very good; everything about him is just amazing,” Jokate
aliliambia jarida la Mzuka.
Aliliambia jinsi ambavyo Diamond alikuwa akimfanyia surprise nyingi na mapenzi tele.
“The
first one I think is buying me a car coz sikuexpect, I didn’t see it
coming, ilikuwa out of the blue. Unajua tumeshazoea kwamba watu
wanaofanya vitu hivi ni wanaume wakubwa, wababa mpaka uhongwe umehongwa
na mtu mzima lakini for Diamond amesema hivyo tu ghafla…. nilikuwa sijui
natoka naenda wapi akaniambia hebu njoo nikuambie he said, ‘I got you a
car, he gave me money akasema go and buy that car,” alisema na kuongeza
kuwa Diamond alimkabidhi shilingi milioni 15 kununua gari hilo.
“He
said go buy this car. Ananiulizaga, he is very funny’ unapenda gari
fulani mi’ mimi najibu yeah I like it’. I was so shocked, ghafla so I
think that’s the first surprise. He is too sweet; kwanza he will come
take you out for a dinner out of the blue. Yaani anafanya vitu ambavyo
kwa age yake na persona yake vilivyo alivyo an artist unategemea awe
ghetto, ‘ebwana uko wapi twenzetu pale tukapige kiepe’ unajua vile. But
he is very sweet that surprises me, he surprises me I think every day.
Na anachonisurprise kingine kikubwa I will tell you guys, ni uwezo wake
wa kufikiri, he is very smart.”
Bahati
mbaya kuamini huko kumekuja kugeuka baada ya hivi karibuni Diamond
kurudiana na Wema Sepetu na ukweli huo ulibainika baada ya kuvuja picha
zao wakiwa Hong Kong hivi karibuni. Tukio hilo liliuvunja vibaya moyo wa
Penny ambaye tayari alikuwa akiishi na Diamond na nyumbani kwao alikuwa
akijulikana na mchumba aliyepitishwa na familia nzima akiwemo mama yake
Diamond na dada zake.
Usaliti
huo ulipelekea mgogoro mkubwa kati ya Diamond na Penny ambaye kuna
tayari kuna tetesi kuwa wameshaachana rasmi. Tangu hapo Wema amekuwa
haoni aibu kuonesha mapenzi yake kwa Diamond ikiwa ni pamoja na
kupromote show ya Diamond ya Christmas.
Kwenye
show hiyo ya Jumatano hii ndipo mambo yalipowekwa wazi zaidi ambapo
Wema alikuwa mmoja wa watu waliopanda kwenye stage na kuongea na watoto
waliokuwa wakishuhudia show. Kwenye show hiyo Diamond alisikika
akiuliza: Mnataka kumjua mchumba wangu”? Baadaye wakati akitaka kuimba
wimbo wake ‘Ukimwona’, hitmaker huyo aliuliza tena: Naskia ninayetaka
kumuimbia wimbo huu yupo humuhumu ndani,” na ndipo Wema Sepetu akapanda
kwenye stage wakaimba na kucheza wote.
Baada
ya Penny, hatujui ni msichana gani atakayevunjwa tena moyo na Diamond
kutokana na kuendelea kwa uhusiano usiokatika na Wema kama vile wamekula
yamini
No comments:
Post a Comment