ABIRIA wa
daladala moja namba T608 BKP aina ya Toyota Hiace eneo la Gongo la
Mboto jijini Dar es Salaam leo wamenusurika kifo baada ya gari hiyo
iliyokuwa ikielekea Moshi-Baa kupata ajali ikiwa inawakimbia wafanyakazi
wa SUMATRA, ajali hiyo imetokea leo majira ya jioni baada wa dereva wa
daladala hiyo kuona gari la Sumatra na kuanza kutimua mbio bila kujali
usalama wa abiria.
Dereva
huyo aliyekuwa anatumia barabara za pembezoni mwa barabara kuu alianza
kuendesha gari hilo kwa kasi na baada ya askari kumuona walimfuata na
kumzuia ili wamuhoji baada ya kuzuiwa kwa mbele gafla aliondoa gari kwa
kasi na kuingia uchochoro mwingine kisha kutaka kuingia barabara kubwa
kwa kasi ndipo alipogogana na gari lingine dogo lililokuwa likipita.
Kama
vile mchezo wa kuigiza wa mbio za magari dereva huyo aliwasha tena gari
hilo likiwa tayari limeumia na kutaka kukimbia kwa kasi ndipo
lilipomshinda na hatimaye kuingia mtaroni na kukwama. Ghafla dereva huyo
alishuka kwenye gari na kuanza kutimka lakini askari na baadhi ya
wananchi walimtia mikononi baada ya hatua chache ndipo wananchi wenye
hasira wakaanza kumpiga hadi walipo zibitiwa na askari waliofika eneo la
tukio hilo muda mfupi.
Abiria
walianza kujinusuru kwa kutoka ndani ya gari hilo wakikimbia huku
wengine wakitokea madirishani. Hata hivyo mmoja wa abiria alizimia
kutokana na tukio hilo hivyo kukimbizwa hospitalini kwa msaada zaidi.
Baadhi ya mashuhuda waliozungumza na mtandao huu walisema dereva huyo
alikuwa akiwakimbia Sumatra kwani daladala hiyo ilikuwa ni bubu hivyo
alihofia kukamatwa ndipo alipoanza kutimua mbio hovyo. Hata hivyo hakuna
abiria aliye jeruhiwa kwa ajali zote mbili zilizotokea wakati gari hilo
likitimua mbio.Credit: The Habari.com
No comments:
Post a Comment