by Gordon Kalulunga
TANGU niwe mmoja wa waandishi wa
habari 5 waliobahatika kufauru usaili kati ya waandishi 72 Tanzania na
kujifunza na kubobea kuandika habari za afya ya uzazi nchini Tanzania tangu
mwaka 2012 nimejionea, nimesikia, nimegusa, nimenusa wakati mwingine kuyaishi
maisha na wanawake wajawazito na hata ambao bado hawajawa wajawazito…
Nieleze wazi kuwa mafunzo hayo
niliyapata kupitia program ya Fellowship inayoratibiwa na mfuko wa vyombo vya
habari Tanzania maarufu kama Tanzania Media Fund (TMF) na kufundishwa na
madaktari bingwa wa masuala ya afya ya uzazi.
Moja ya mambo ambayo nilijifunza
kutoka kwa wataalamu hasa madaktari nikiwa field, kusoma mitandao na baadhi ya
wanawake waliosema wazi wazi kuhusu dalili za ujauzito na kati ya nyingi
nilizoelezwa kati yake 13 nimeona nikushirikishe katika makala hii ya
uchambuzi.
Mwanamke anapopata ujauzito kwa
kawaida huwa anaanza kuona dalili ambazo si za kawaida. Na ni wakati huo ambao
ni muafaka kwake kuanza kuuchunguza mwili wake.
Inaonesha kuwa homoni zinazosambaa
mwilini mara tu unapopata ujauzito husababisha mabadiliko kadhaa katika mwili
wake ambayo yanaweza kugundulika kabla hata ya uchunguzi halisi wa kujua kama
mjauzito au la.
1. Maumivu kwenye
matiti.
Hii ni dalili ya kawaida ya ujauzito ambapo nguvu za homoni mwilini huongezeka wakati yai linavyopata “rutuba”, jambo ambalo huongeza wingi wa damu na kuyafanya matiti ya mwanamke kuvimba na kuwa makubwa isivyo kawaida.

2. Maumivu mwilini
Baadhi ya wznawake wanajisikia maumivu kama vile wanataka kuingia katika siku zao. Kwa kawaida hali hii hutokea wakati yai likiwa linasafiri kwenda katika chumba cha mimba. Hivyo, hali hiyo husababisha sehemu hiyo itanuke taratibu na kusababisha maumivu hayo.

3. Kutokwa damu bila
kutegemea
Wanawake wengi hufikiria kutokwa na damu kidogo ni dalili ya kuwa katika siku zao. Lakini, katika hali halisi, kutokwa damu kusikotegemewa, huwakumba asilimia 25 ya wanawake wakati wa kurutubika kwa yai na iwapo utaona hedhi inakuwa fupi au inafanyika katika hali ambayo si ya kawaida, mwanamke anashauriwa kwenda kufanya kipimo cha ujauzito au kujipima mwenyewe na kifaa cha kupimia ujauzito..

4. Kuchoka
Mwanamke anapojisikia kuchoka na kukosa raha, au kutaka hata kulala wakati akiwa kazini, wakati huo mwili wake unakuwa unajirekebisha kuingia katika kipindi kipya cha mabadiliko.

Inaelezwa kuwa katika kipindi cha
mwanzo cha ujauzito ni muda ambao mtoto tumboni huanza kutumia sehemu ya nguvu
za mwanamke na hivyo kumletea uchovu na usingizi.
5. Chuchu kuwa nyeusi
Chuchu huanza kubadilika rangi yake kutokana na chembechembe za uhai (seli) kuanza kufanya kazi kwa nguvu zaidi hata hivyo wanawake wenye ngozi nyeusi hawawezi kuiona dalili hii mapema hadi muda wa kama wiki kumi zipite.

6. Kichefuchefu
Hali hii huwapata asilimia 85 ya wanawake wanapopatwa na ujauzito, ambapo nyakati za asubuhi ndipo hasa hujionyesha.

7. Mwili kuvimba
Kuna wakati kupungua kwa nguvu za uyeyushaji
chakula kunaweza kumsababishia mwanamke kuona tumbo limevimba na nguo zikawa
zinambana kutokana na chakula kujaa katika utumbo. Lakini hali hiyo ikiendelea
na ukaona siku zako haziji, basi ni vyema ukatambua kwamba tayari una ujauzito
na kinachokupasa ni kwenda kuhakikisha.
8. Kwenda haja ndogo
mara kwa mara
Mwanamke kwenda haja ndogo kila mara ni dalili kwamba kibofu kimeanza kufanya kazi ya ziada, ambapo huwa kinafanya kazi ya kuondoa maji kwa uthabiti zaidi wakati wa ujauzito.

Hali hii pia hujitokeza mwishoni mwa
ujauzito, ambapo kibofu kitakapokuwa kinarudia hali yake ya kawaida baada ya
kufanya kazi kwa muda mrefu.
9. Tamaa ya vitu
mbalimbali
Kutokana na mwili kuwa na “mzigo” wa ujauzito na hivyo kuchoka, hali hiyo humfanya mwanamke kutamani vitu mbalimbali ili kukidhi mabadiliko yaliyojitokeza katika mwili wake. Hii ni pamoja na kutaka vyakula fulani au kufanya mambo ambayo hapo nyuma alikuwa hayapendi.

10. Kuumwa kichwa
Kuongezeka kwa damu kunaweza kusababisha kichwa kuuma japokuwa si sana, hususani katika wiki za mwanzo za ujauzito. Hata hivyo, hali hii hukoma mwili unapojirekebisha na mzunguko wa homoni unaotokana na ujauzito.

11. Kufunga choo.
Homoni ambazo husababisha mwili kuvimba pia husababisha kufunga choo kutokana na mfumo wa kuyeyusha chakula kutofanya kazi vyema. Hata hivyo hali hii inaweza kujitokeza zaidi wakati ujauzito unapoendelea kukua.

12. Kuwa na hasira
‘’Kutokana na kuongezeka kwa homoni za utendaji kazi mwilini, hali hiyo itakusababishia uchovu, na kukufanya kuwa na hasira,”anasema Melissa Goist, Profesa na Mtalaama wa Masuala ya Uzazi wa Chuo Kikuu cha Ohio, Marekani.

13. Kuongezeka kwa joto
mwilini Kipimo cha joto la mdomo ni muhimu katika kutambua hali ya
ujauzito. Kwa kawaida joto huongezeka kwa nyuzi moja au zaidi wakati yai likiwa
linatunga mimba. Hali hiyo ikiendelea kwa zaidi ya wiki mbili, itakuwa
inaonyesha dhahiri kwamba kuna “mtoto anakuja”.
No comments:
Post a Comment