Nahodha wa klabu ya Manchester United Nemanja Vidic
amethibitisha rasmi kwamba ataondoka Manchester United baada ya msimu wa huu kuisha.
Katika taarifa yake aliyotoa kwa mtandao rasmi wa
ManUtd.com, beki huyo kutoka Serbia alisemathe: “Ni mwaka wa mwisho wa mkataba
wangu na nimekuwa na miaka nane mizuri nikiwa hapa. Muda wangu katika klabu hii
kubwa siku zote utabaki kuwa kumbukumbu yangu zaidi katika maisha yangu ya
soka.
“Sikuwahi kufikiria kama ningeshinda makombe 15 na kwa
hakika sitousahau usiku ule mkubwa jijini Moscow, kumbukumbu zile nitaishi nazo
milele. Hata hivyo, nimefikia uamuzi kwamba nitaondoka klabuni mwishoni mwa msimu
huu. Nataka kujipa changamoto mpya kwa mara nyingine na kujaribu kufanya vizuri
zaidi katika miaka ijayo.
“Sifikirii kuendelea kubakia England kwa sababu klabu
pekee ambayo nilitaka kuichezea nchi hii ni Manchester United na nilipata
bahati kubwa ya kuwa sehemu ya klabu hii kwa miaka mingi. Nina machaguo kadhaa
na nitachagua chaguo la timu nzuri kwangu na familia yangu.
“Kwa sasa nitaweka umakini na jitihada zangu zote
katika kuichezea Manchester United na kujituma kwa kila hali mpaka mwisho wa
msimu.Natumaini taarifa hii inatosha kuachwa kusambaza tetesi zozote kuhusu
hatma yangu.”
No comments:
Post a Comment