


INAWEZA kukushtua lakini ndivyo ilivyotokea.
Kichanga cha siku thelathini, Veis Venus
kiliibwa hivi karibuni, mtuhumiwa akiwa ni
mwanamke aliyetajwa kwa jina moja la Grace
akidaiwa ni mjamzito feki.
Kichanga cha siku thelathini, Veis Venus
kiliibwa hivi karibuni, mtuhumiwa akiwa ni
mwanamke aliyetajwa kwa jina moja la Grace
akidaiwa ni mjamzito feki.
Mtoto Veis Venus aliyekuwa ameibiwa.
Tukio hilo la kushangaza lilijiri Januari 27, 2013
maeneo ya Posta jijini Dar na mtoto huyo
kupatikana Januari mwaka huu, mkoani Mbeya.
Akizungumza na waandishi wetu juzi nyumbani
kwake, Kawe ya Tanganyika Parkers, Dar, mama
mzazi wa mtoto huyo, Salma alisimulia kisa
kizima:
“Ilikuwa Januari 24, mwaka jana, marafiki
zangu watatu walikutana na mwanamke
aliyesema ana taasisi inayotoa misaada kwa
watoto.
“Kwa sababu nilihitaji, nikambeba mwanangu
na kwenda Mwenge ambako nilionana na
mwanamke huyo aliyejitambulisha kwa jina la
Grace.
Mama akiwa na mwanaye Veis Venus.
“Aliniambia asingetoa msaada mpaka Sikukuu
ya Krismasi na Boxing Day zipite. Januari 27
nikakutane naye.
”Cha kushangaza siku hiyo sikumkuta Grace
bali mwingine aitwaye Suzana. Alisema ni
mfanyakazi wa Grace.
“Siku hiyo nilikuwa na mwanamke mwingine
naye ana mtoto. Suzana akatuambia wana ofisi
Mlimani City na Posta, hivyo tulitakiwa kwenda
Posta kupokea misaada hiyo.
“Kufika kituoni, Suzana akashauri mimi na
mwenzangu tupande daladala, yeye na watoto
wetu wapande Bajaj tukakutane Posta.
“Dakika chache mbele akabadili kauli, akasema
yeye aondoke na mtoto mmoja tu na
alimchagua mwanangu.
Mama mtoto.
“Tulipanda daladala mpaka Posta ambapo
tuliwasiliana na Suzana akasema yupo kwenye
foleni. Tulimsubiri kwa muda, tulipompigia
tena simu yake ikawa haipatikani.
“Ilibidi tumpigie simu Grace, akasema Suzana
alipitia Kigamboni kuchukua misaada hivyo
tumsubiri. Tuliendelea kusubiri hadi saa kumi
na mbili jioni, hakuna aliyekuwa akipatikana
kwenye simu,” alisema Salma.
Salma: Nililia sana jamani! Nilisema moyoni
sitaki tena msaada namtaka mtoto wangu lakini
hakuwepo. Niliwapa habari ndugu kisha
tukaenda kutoa taarifa Kituo cha Polisi cha
Kawe na Kituo cha Polisi Sitakishari jijini Dar
kwa vile mtu wa kwanza kuniambia habari za
msaada anaishi huko.
Naye shangazi wa mtoto huyo aliyejitambulisha
kwa jina moja la Selina alikuwa na haya ya
kusema:
“Baada ya kupokea habari kutoka kwa Salma
tulichukua namba za wale wezi na kwenda nazo
kampuni moja ya simu kuziangalia.
“Desemba 30, mtu wa kampuni hiyo
aliwaambia polisi, Suzana yupo Mbeya. Januari
18, bila kutarajia, Grace na Suzana wakatiwa
mbaroni huko Mbeya. Grace alidai eti mtoto ni
wake.
“Januari 19, polisi waliwachukua wote na
kurudi nao Dar kwa ajili ya vipimo vya DNA vya
Grace, Salma na mtoto Veis.
“Baada ya vipimo, majibu yalionesha mtoto ni
wa Salma huku Grace na Suzana wakiwekwa
chini ya ulinzi wa polisi na kufanya taratibu za
kuwafikisha mahakamani kujibu tuhuma hizo,”
alisema Selina.
Habari za kipolisi zinadai kuwa, Grace
alipobanwa zaidi alisema alimwiba mtoto huyo
kwa vile hakuwahi kuzaa na kwamba
alimdanganya mumewe (hakumtaja jina)
anayeishi Rukwa kwamba ana mimba hivyo
alikuwa Mbeya kujifungua.
No comments:
Post a Comment