Linapokuja
suala la mwenzi wa kufunga nae pingu za maisha, wengi hutaja sifa
zinazotofautiana na sifa za boyfriend ama girlfriend wanaetaka kuwa naye.
“Kuishi
na mwanaume mwenye meno 32, hukutoka naye familia moja, sio rahisi.” Aliwahi
kusema mchungaji ambaye pia ni mbunge mwanamke aliyeteuliwa na Rais.
“Mimi
nampenda mwanaume mchapakazi, anayempenda Mungu. Mwanaume mweusi, mwembamba
lakini asiwe mwembamba sana…kawaida.” Shilole amefunguka.
Hata
hivyo, Shilole ambaye ana watoto wawili amesema kuwa kwa sasa hana mpango wa
kuolewa.
“Watoto
tayari ninao wawili, sina mpango wa kuolewa. Kuolewa ni maamuzi ila bado
sijaamua, nikiamua ntaolewa tu.”
Shilole
ambaye mwaka jana alifanikiwa kupata show nchini Uingereza, ameachia wimbo wake
unaoitwa ‘Chuna Buzi’ na mashabiki wa muziki wake wanaonesha kuulewa.
No comments:
Post a Comment