Mkuu wa idara ya
Mauzo na Usambazaji wa Vodacom Julius Kastabu (Kushoto) akikabidhi msaada wa
chakula kwa Mkurugenzi wa kituo cha kulea watoto yatima cha Sifa Group Children
Foundation Center kilichopo Bunju, Dar es Salaam, Bi. Sifa John ikiwa ni sehemu
ya msaada kutoka kwa wafanyakazi wa kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom
Tanzania.
Wafanyakazi
wa Vodacom Tanzania kutoka kushoto ni Happiness Macha na Elihuruma Ngoi
wakisaidia kushusha msaada wa chakula iliyotolewa na wafanyakazi wa
Idara ya Mauzo na Usambazaji wa kampuni hiyo kwa kituo cha kulea watoto
yatima cha Sifa Group Children Foundation Center kilichopo Bunju, Dar es
Salaam kupitia kampeni ya Pamoja na Vodacom.
Wafanyakazi
wa Idara ya Mauzo a Usambazaji wa kampuni ya simu ya Vodacom Tanzania,
wakiwa kwenye picha ya pamoja wakati walipotembelea na kukabidhi msaada
mbali mbali kwa kituo cha kulea yatima cha Sifa Group Children
Foundation Center kilichopo Bunju, Dar es Salaamkupitia kampeni ya Pamoja na Vodacom.
Mkurugenzi wa kituo cha kulelea yatima
cha Sifa Group Foundation Children Center kilichopo Bunju mkoani
Dar Es Salaam ametoa wito kwa wadau mbali mbali nchini kuwa tayari kujitolea
kusaidia vituo vya watoto yatima kikiwemo kitu chake ili kuweza kutatua
matatizo yanayokabili vituo vingi nchini ikiwemo uhaba wa madarasa ya
kujisomea, ubovu wa vyoo na malazi.
Hayo yalibainishwa na Mkurugenzi huyo wakati akipokea misaada
kutoka kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania kupitia taasisi yake ya
Vodacom Fondation iliyojumuisha vitu mbali mbali ikiwemo magodoro, vifaa vya
shule, vyombo vya ndani, vyakula pamoja na ada za shule kwa watoto wa kituo
hicho.
“Tuna tatizo la uhaba wa fedha ili kuweza kumalizia kituo chetu
kipya ambacho tumejitaidi kupata kiwanja hadi sasa lakini bado hatujapata fedha
zakuweza kujengea kituo hicho, vile vile tunahitaji tujenge madarasa ambayo
yatasaidia watoto wetu kujisomea lakini fedha hatuna zakuweza kufanikisha mradi
huo.”
“Tunapokea watoto wengi ambao hawana uwezo wa kusoma wala
kuandika tumechukua jukuma la kuwafundisha hapa kwa uwezo mdogo tulionao na
darasa hili dogo ambali haliwatoshi na pia halina vifaa kamili vya kufundishia,
tunawaomba wadau wajitolee kutusaidia ili tuweze kutoa elimu kwa watoto hawa
amba ndio msingi pekee wa kuwapatia ili wajiendeleze katika maisha a
Yao.”
Mkurugenzi huyo alitanabaisga kuwa, “Tumekuwa tukilalamika siku
hadi siku kuhusiana na ubovu wa vyoo tulio nao ambao mara kwa mara husababisha
maradhi mbalimbali kwa watoto kutokana na wingi wa watoto kuto kuendana na
idadi ya vyoo wanavyotumia ni vichache hivyo inakuwa vigumu kuviweka vikiwa
visafi wakati wote,”.Alisema
Kwa upande wake Ofisa Mkuu wa Mauzo na Usambazaji wa Vodacom
Tanzania, Hassan Saleh wakati wa makabidhiano ya misaada hiyo ameeleza kuwa ni
jambo la busara wao kama kampuni kusaidia kutatua matatizo yaliyondani ya jamii
kwani wao ndio wanaowaunga mkono kila siku.
“Tunaamini misaada tuliyoitoa itaweza kusaidia watoto hawa kwa
namna moja au nyingine, tunatambua changamoto wanazokumbana nazo lakini sisi
kama kampuni tuataendelea kuhakikisha tunasaidia jamii kadri tuwezavyo, hiyo
imekuwa ni jadi yetu na hatuwezi kuicha.”Alisema Saleh
Mmoja wa watoto anaelelewa katika kituo hicho Shantala Mussa
aliwashukuru wafanyakazi wa kampuni hiyo kwa kutoa sehemu ya fedha zao na
kuwasaidia kwa kuwaletea misaada hiyo na kuwaomba waendelee na moyo huo huo wa
kujitolea na kutoa wito kwa makampuni mengine kuweka mazoea yakujitolea ili
kuweza kuwafanya watoto yatima wasahau matatizo wanayokumbana nayo na kujihisi
nao ni watoto wanaohitaji matuzo kama watoto wa kawaida.
No comments:
Post a Comment