AMEKUWA akionekana kwa nadra kocha Andre Villas-Boas tangu atupiwe virago Tottenham mwezi uliopita.
Lakini
inasemekana anaweza kuwa tayari kurudi kazini, baada ya kuonekana
akizungumza na kocha wa Bayern Munich, Pep Guardiola katika kambi ya
timu hiyo ya Ujerumani mjini Doha, Qatar.
AVB alionekana mtulivu na mwenye furaha wakati akijadiliana masuala ya kiufundi na Guardiola kwa muda mrefu.
Kikao: Andre Villas-Boas (kulia) akizungumza na kocha wa Bayern, Pep Guardiola (kushoto) katika kambi ya mazoezi Doha
Maelekezo: Guardiola akimuelekeza jambo Villas-Boas
Guardiola na Villas-Boas walizungumza kwa muda mrefu Doha
Kocha
huyo wa zamani wa Spurs na Chelsea pia alikutana na nyota wa Bayern,
Franck Ribery, Thiago Alcantara, Dante Bonfrm na Claudio Pizarro
mwishoni mwa mazoezi hayo.
Lakini
AVB hakuishia tu kwenye kambi ya Bayern, kwani pi alikutana na gwiji wa
Hispani na Real Madrid, Raul Gonzalez, ambaye alichezea kwa misimu
kadhaa wapinzani wa Bayern, Schalke, aliyetembelea mazoezi ya timu hiyo.
Ilikuwaa ni safari fupi kwa Raul kufika kwenye kambi hiyo ya mazoezi, ambaye kwa sasa anachezea Al Sadd ya ligi Kuu ya Qatar.
Villas-Boas (wa pili kulia) alikutana na wachezaji Franck Ribery na Dante Bonfim baada ya mazoezi
Thiago Alcantara (wa pili kushoto) alikwenda kumsalimia kocha wa zamani wa Spurs
Claudio Pizarro (wa pili kushoto) pia alihakikisha anamsalimia na kuzungumza naye kidogo Villas-Boas
Gwiji wa Hispania, Raul, anayechezea Al Sadd ya Qatar, aliungana na AVB katika kambi ya mazoezi
No comments:
Post a Comment